Thursday, 3 March 2016

Jipu la wanaotumia majina feki Mitandaon Kutumbuliwa

Mahakama
Watu wanaobuni majina bandia katika mitandao huenda wakakabiliwa na mashtaka kulingana na maelezo yaliopendekezwa na waendesha mashtaka nchini Uingereza na Wales.
Huduma ya waendesha mashtaka inasema watu wazima ni lazima washtakiwe iwpo watatumia majina bandia katika mitandao ya kijamii ili kuwanyanyasa wengine.
Pia watu wanaoweka machapisho yasio na heshima ya uongo na kusababisha dhiki na wasiwasi pia watashtakiwa.

Huduma hiyo pia inayafanyia marekebisho maelezo yao ili kuhakikisha kuwa wafanyikazi wake wanaelewa uhalifu wa kisasa.
''Majadiliano ya wiki sita kuhusu marekebisho hayo yameanza ,''amesema mkurugenzi wa mashtaka ya uma Alison Sanders.
Matumizi mabaya ya mtandao ni kutokana na uoga lakini unaweza kuwa na athari mbaya kwa wanaolengwa.
Hatahivyo huduma hiyo imesema kuwa watoto hawatafunguliwa mashtaka kutokana na ukosefu wa kujua mabaya na mazuri.

No comments: