“Ningechukua zote mbili, nilipochukua ile moja nilikasirika, naamini kama ninajua, tuzo za Tanzania haikupita hata kuwa nominated, nilikwenda Nigeria nikiwa na uhakika ninaenda kushinda”, alisema Richie.
Pamoja na hayo Richie amesema sio mtu wa majivuno na kujionyesha kama ilivyo kwa wengine, kwani tuzo hiyo sio ya kwanza kuchukua, kwani alishawahi kuchukua tuzo kubwa zaidi ya hiyo mwaka 2001, pamoja na uvumilivu na bidii ndio umemfikisha hapo.
“Mi sio bishoo bishoo wa kujishaua, nilishawahi kushinda msanii bora wa kiume ya Mnet mwaka 2001, nina history kubwa sana, ukiangalia tangu nilipoanza nina miaka 18 ndio nachukua tuzo nyingine Nigeria, sasa mtu miaka miwili na nusu anataka awe na hela”, alisema Richie.
Pia Richie ameelezea mipango yake ya kufanya kazi na Bishanga ambaye ndiye alimtambulisha kwenye sanaa ya maigizo, na kusema iwapo atapa fursa atafanya naye kazi, kwani ka sasa yuko busy sana na majukumu ya kampuni yake.
“Bishanga yupo, nikiwa serious naweza nikafanya nae kazi, naweza nikampata jumamosi au jumapili, yuko busy sana, hata director wangu anapenda tufanye kazi na Bishanga na sababu zipo za msingi, lakini kama demand ipo basi ni suply tu itakayofuata”, alisema Richie.
Vile vile Richie amejibu tuhuma ambazo wasanii wengi wa filamu wanatuhumiwa kuwa baada ya kifo cha Steven Kanumba tasnia hiyo imeshuka ubora wake, na kusema kuwa tasnia hiyo haiwezi kushuka kwani kila siku wasanii wapya wanaibuka.
“Tasnia haijashuka, hata mimi nikiondoka haiwezi kushuka, tulikuwepo, wakaja wengine kina Kanumba, ni season na time, sio wivu na roho mbaya kwa nini kanumba, mimi Vicent Kigosi 'Ray' jina nilimpa mimi, nikasema utaitwa Ray, na pi nina dicpline”, alisema Richie.
No comments:
Post a Comment