Makaburi matatu yanayotembelewa sana na watu jijini Moscow yatawekewa huduma ya mtandao ya wi-fi.
Wanaotembelea
makaburi hayo wataweza kutumia mtandao wa intaneti bila malipo katika
makaburi ya Novodevichy, Troyekurovskoye na Vagankovo kuanzia mapema
2016 kwa mujibu wa tovuti ya Moscow City.Mkuu wa huduma za makaburi mjini Moscow Artem Yekimov anasema lengo ni kusaidia wageni kwenye makaburi hayo kutafuta habari zaidi kuhusu watu mashuhuri waliozikwa humo.
Aidha, kuwafanya wafurahie matembezi yao makaburini.
Kampuni ya mawasiliano ya YS System inasema ilijitolea kuweka huduma ya wi-fi humo baada ya kusikia mipango ya kutenga maeneo ya watu “kutulia kisaikolojia” katika makaburi hayo.
Makaburi ya Novodevichy ni moja ya maeneo yanayotembelewa sana na watalii Moscow.
Miongoni mwa watu waliozikwa humo ni mwandishi Anton Chekhov, kiongozi wa zamani wa muungano wa Usovieti Nikita Khrushchev na rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltsin.
No comments:
Post a Comment