Sunday 6 December 2015

Polisi: Shambulizi la kisu London ni la 'kigaidi'

Polisi wanasema Aliyemdunga kisu abiria London ni 'gaidi'
Idara ya polisi nchini Uingereza inasema kuwa inalichukulia kisa cha udungaji kisu katika kituo cha gari moshi jijini London, kama tendo la kigaidi.
Mtu mmoja aliyekuwa amejihami kwa kisu aliwashambulia abiria katika kituo cha treni kilichoko eneo la Leytonstone.

Mtu mmoja anatibiwa majeraha mabaya, ilihali wengine wawili wanatibiwa majeraha madogo madogo.
Walioshuhudia wanasema kwamba, alifoka kuwa "Hii ni kwa sababu ya Syria!". Polisi walimpiga kwa mtutu wa bunduki na wakamtia mbaroni.
Taarifa ya polisi inasema kuwa tishio la kigaidi lingalipo.
Mkanda wa video kutoka mahala pa shambulizi hilo inaonyesha bayana kiwango cha damu iliyomwagika katika lango la kituo hicho cha treni cha Leytonstone kilichoko chini ya ardhi.

No comments: