Tuesday 15 December 2015

Chelsea yachapwa tena na Lester City

Wachezaji wa Leicester City wakishangilia ushindi
Mabingwa watetezi wa ligi kuu England Chelsea wamezidi kuwa katika wakati mgumu msimu huu baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Leicester City.
Mshambulijai wa Jamie Vardy ndie aliyeanza kupeleka msiba kwa The blue baada ya kuandika bao la kwanza katika katika ya 34 ya mchezo. Winga Riyard Mahrez akaongeza bao la pili na la ushindi katika dakika ya 48 ya mchezo.

Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Chelsea lilifungwa na Loic Remy aliyefunga kwa kichwa baada ya kupokea krosi nzuri kutoka kwa Pedro'.
Kwa ushindi huu Leicester City wanareje kileleni mwa ligi wakiwa na alama 35 baada ya kucheza michezo kumi na sita huku Chelsea wakijichimbia katika nafasi 16 wakiwa na alama 15 wakiwa wamepoteza michezo tisa katika michezo 16.
Mshambulia Jamei Vardy ameendelea kuongoza katika kinyanyanyiro cha mfungaji bora msimu huu baada ya kuwa amezipasia nyavu mara 15 katika michezo michezo 16 waliocheza.

No comments: