Virusi hai vya Zika vyapatikana katika mate na mikojo ya wagonjwa,wanasayansi wa Brazil wamesema.
Matokeo
hayo hayamaanishi kwamba ugonjwa huo unaweza kusambazwa kupitia maji
maji hayo ya mwilini.Sababu kuu ya kuenea kwa virusi hivyo ni kupitia
kuumwa na mbu,lakini wanasayansi wanachunguza njia nyengine.Huku maambukizi ya Zika yakiwa sio makali,ugonjwa huo umehusishwa na maelfu ya watoto waliozaliwa na kasoro.
Virusi vya Zika pia vimepatikana katika majimaji mengine ya mwilini katika mripuko mwengine uliotokea eneo la Polynesia,lakini mamlaka ya Brazil inasema kuwa hii ni mara ya kwanza virusi hai vya Zika kupatikana.
Paula Gadelha,mkuu wa taasisi ya Fiocruz ambayo inashirikiana na wizara ya Afya amesema:''Virusi hivyo vya Zika vimepatikana katika Mate na mikojo''.
No comments:
Post a Comment