Mkuu wa kanisa
katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa wazo la mgombea wa kiti wa
chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump la kujenga ukuta kati
ya Mexico na Marekani si la kikristo.
Papa Francis alisema kuwa
kwa mtu yeyote ambaye katika karne hii ya 21 anayetaka kujenga ukuta
badala ya kujenga daraja huyo si Mkristo.Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.
Trump ambaye anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republicans katika uchaguzi mkuu ujao amependekeza kujenga ukuta na ua katika mpaka kati ya nchi yake na mexico ilikuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.
Hilo haliambatani na mafunzo ya injili
"Sharti tutathmini matamshi yake '' tunapaswa kuchunguza kwa kina ''
Bwanyenye Donald Trump kwa upande wake amesema kuwa papa Francis hana haki yeyote kumhukumu iwapo ni muumini au la ''inasikitisha'' alisema Trump.
Mmoja kati ya wamarekani 5 ni wakatoliki.
Papa Francis ni maarufu sana nchini Marekani
No comments:
Post a Comment