wapiganaji wa islamic state mjini Raqqa |
Mashambulio ya
Ufaransa na mataifa mengine dhidi ya ngome ya Islamic State huko Raqqa
nchini Syria siku ya jumapili yamewauwa takriban wapiganaji
33,wanaharakati wamesema.
Kundi la wapiganaji wa haki za
kibinaadamu kutoka Syria limesema kuwa wengi walifariki wakati vituo vya
kukagua watu vilivyoshambuliwa.Hatahivyo chombo kimoja cha habari kinachohusishwa na IS kimesema kuwa hakuna majeraha yoyote yaliotekelezwa na mashambulio hayo.
Kundi hilo la haki za kibinaadamu nchini Syria ambalo lina wanahabari wake nchini humo,limesema kuwa wapiganaji 33 waliaminika kuuawa katika mashambulio hayo,lakini miili yao iliharibiwa vibaya hali ya kuwa haiwezi kutambulika na hivyobasi haliwezi kutoa idadi sawa ya waliouwawa
No comments:
Post a Comment