Rais wa Equatorial
Guinea Teodoro Obiang Nguema, ambaye ameongoza taifa hilo kwa miaka 36,
amesema atawania tena, shirika la habari la AFP limeripoti.
Kiongozi
huyo mwenye umri wa miaka 73 alisema kupitia kituo cha redio cha taifa
kwamba ameungwa mkono na chama chake kuwania urais kwa muhula mwingine
wa miaka saba mwaka ujao.Chama cha Obiang cha Democratic Party of Equatorial Guinea kilishinda viti 99 kati ya 100 vya ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2008.
Alishinda uchaguzi wa urais mwaka mmoja baadaye kwa kupata 95% ya kura.
Obiang ni mmoja wa viongozi waliokaa madarakani muda mrefu zaidi Afrika.
No comments:
Post a Comment