Serikali ya Marekani imetoa
tahadhari ya kusafiri duniani kote kwa raia wake, ikiwaonya kuwepo kwa
ongezeko la tishio la kigaidi.
Tahadhari hiyo inasema taarifa
zilizopo hivi sasa zinaashiria kwamba makundi kama vile Islamic State,
al-Qaeda na Boko Haram wanaendelea kupanga mashambulio katika maeneo
tofauti.Inawataka wasafiri kuwa makini hasa wanapokuwa katika mikusanyiko ya watu au pindi wanapotumia usafiri wa umma.
Hata hivyo, afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameiambia bbc kwamba hakuna sababu ya kuamini kwamba raia wa Marekani ndio walengwa.
Mamilioni ya raia wa marekani watasafiri wiki hii kwa ajili ya sikukuu ya kutoa shukrani siku ya alhamisi.
No comments:
Post a Comment