Thursday, 26 November 2015

Man U yajiweka pabaya kusonga mbele UEFA

Man U vs PSV
Kikosi cha Manchester United bado kipo kwenye wakati mgumu kuhakikisha kinafuzu hatua ya mtoano ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya kufuatia ulazimishwa sare ya bila kufungana na ya timu ya PSV kwenye uwanja wa Old Trafford mchezo uliopigwa usiku wa Jumatano November 25, 2015.
Ulikuwa ni usiku wa aina yake kwa upande wa United ambao walitawala mchezo huo kwa kila idara lakini hawakufanikiwa kutumbukiza mpirakwenye nyavu za wapinzani wao.
Jesse Lingard alipana nafasi nzuri ya kufunga  lakini mpira ukagonga mwamba huku shuti la Morgan Schneiderlin likiokolewa.

Manchester United watafuzu hatua ya 16 bora ikiwa watafanikiwa kuifunga timu ya Wolfsburg kwenye mchezo wao wa mwisho wa kundi B kwenye mchezo utakaopigwa December 8, 2015.
Timu tatu za kuni hilo ambazo ni Wolfsburg, Manchester United na PSV zote zinanafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo kutokana na tofauti ya pointi zao. Wolfsburg ndiyo vinara wa kundi hilo wakiwa na pointi tisa wakifuatiwa na United wenye pointi nane huku PSV wao wakiwa nafasi ya tatu kwa pointi zao saba.
United walikuwa wakifahamu fika kuwa ushindi pekee kwenye mchezo dhidi ya PSV ungewapa tiketi ya kusonga mbele kwenye hatua ya mtoano lakini sare imewaacha kwenye wakati mgumu.
Mchezo wa mwisho wa PSV utakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Philips Stadion dhidi ya CSKA Moscow ambao tayari wameshaondoshwa kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa bao 2-0 wakiwa kwao na Wolfsburg.

No comments: