Rais wa Nigeria
Muhammadu Buhari ametoa amri kushikiliwa kwa afisa wa juu anayetuhumiwa
kwa wizi wa zaidi ya dola bilioni mbili zilizotarajiwa kununua silaha za
kukabiliana na wapiganaji wa Boko Haram.
Afisa huyo Sambo Dasuki alikuwa mshauri wa masuala ya usalama ya taifa kipindi cha utawala wa Rais aliyemaliza muda.Dasuki anatuhumiwa kutoa mikataba ya udanganyifu katika ununuzi wa Helikopita ndege za kivita nne na ununuzi wa milipuko kwaajili ya kukabiliana na kundi la Boko Haram.
Amekanusha madai hayo,hatua ya Rais Buhari kuagiza kiongozi huyo achukuliwe hatua ni moja ya jitihada zake katika kutokomeza tatizo la rushwa na makundi ya wapiganaji wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Katika vita dhidi ya ugaidi,Nigeria miezi michache iliyopita majeshi ya serikali yalifanikiwa kurejesha mikononi mwa Serikali maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na Boko Haram.
No comments:
Post a Comment