Friday, 27 November 2015

Mtoto mchanga apatikana katika hori la kanisa moja mjini New York Marekani

Mtoto mchanga apatikana katika hori la kanisa moja mjini New York Marekani
Zaidi ya miaka 2000 iliyopita, Yesu Kristu alizaliwa kwenye hori mjini Bethlehem.
Na katika tukio ambalo ni linafanana na hilo mtoto mdogo ambaye alikuwa kwenye hori amepatikana ndani ya kanisa moja mjini New York.
Inaaminika kuwa mtoto huyo mchanga ambaye ni mvulana aliachwa na mama yake, katika eneo takatifu la kanisa hilo siku ya Jumatatu jioni.
Mtoto huyo alipatikana na padre Christopher Heanue anayesimamia kanisa hilo.
Padre huyo amesema alishangazwa sana na tukio hilo ila alijawa na huruma nyingi.
Amesema kanisa ni mahala ambako watu wanaohitaji misaada na makao huenda na kwa kuwa papa Francis amekuwa akihubiri na kuhimiza waumini wote wawe na huruma, na zaidi ya yote mwaka huu ni mwaka wa huruma, amefarajika sana kuumpa mvulana huyo matumaini na mahala pa kuishi kwa kuwa anahitaji huruma na malezi.

Inaaminika kuwa mtoto huyo alikuwa amezaliwa chini ya saa tano wakati alipopatikana ndani ya kanisa hilo.
Mapadre wa kanisa hilo walimpeleka hospitalini kwa uchunguzi na inasemekana kuwa mtoto huyo yuko katika hali nzuri kiafya.
Askofu wa jimbo na New York Octavio Cisneros amesema mtoto huyo alikuwa amefunikwa na taulo na alikuwa akilia ishara tosha kuwa alikuwa salama wa siha .

 
Askofu wa jimbo na New York Octavio Cisneros amesema mtoto huyo alikuwa amefunikwa na taulo na alikuwa akilia ishara tosha kuwa alikuwa salama wa siha
Aidha alikuwa akipumua vyema na rangi yake ilikuwa sawa na kuwa waligundua kitovu chake hakikuwa kimekatwa.
Chini ya sheria za mji wa New York, kanisa ni mahala salama ambako mtu anaweza kumuacha mtoto wake ambaye ana zaidi ya siku thelathini.
hata hivyo mama wa mtoto huyo ni sharti amjulishe mtu yeyote kuwa amemuacha mtoto ndani ya kanisa ili awajulishe wasimamizi wa kanisa hilo au maafisa wa utawala.
Mama mzazi wa mtoto huyo tayari amepatikana na amehojiwa na polisi.
Mwendesha mashtaka wa mji huo amesema mama huyo hatafunguliwa mashtaka yoyote ya kihalifu kwa sababu alimucha mtoto wake katika hali nzuri na eneo linalokubalika kisheria

No comments: