Tuesday 24 November 2015

Marekani yatoa tahadhari kwa raia wake

Tahadhari ya kusafiri na mashambulio ya kigaidi
Serikali ya Marekani imetoa tahadhari ya kusafiri duniani kote kwa raia wake, ikiwaonya kuwepo kwa ongezeko la tishio la kigaidi.
Tahadhari hiyo inasema taarifa zilizopo hivi sasa zinaashiria kwamba makundi kama vile Islamic State, al-Qaeda na Boko Haram wanaendelea kupanga mashambulio katika maeneo tofauti.

Inawataka wasafiri kuwa makini hasa wanapokuwa katika mikusanyiko ya watu au pindi wanapotumia usafiri wa umma.
Hata hivyo, afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameiambia bbc kwamba hakuna sababu ya kuamini kwamba raia wa Marekani ndio walengwa.
Mamilioni ya raia wa marekani watasafiri wiki hii kwa ajili ya sikukuu ya kutoa shukrani siku ya alhamisi.

No comments: