Friday, 27 November 2015

Wizara ya ulinzi ya China yaidhinisha mpango wa kuunda kambi ya jeshi nchini Djibouti

China kuunda kambi ya jeshi nchini DjiboutiWizara ya ulinzi ya China yaidhinisha mpango wa kuunda kambi ya jeshi nchini Djibouti

Wizara ya ulinzi ya China imetangaza kuidhinishwa kwa mpango wa kuunda kambi ya jeshi katika nchi ya Djibouti.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Wu Chien, alifahamisha lengo la kuundwa kwa kambi hiyo kuwa ni kusaidiana na UN kwa ajili ya kutoa misaada ya kibinadamu katika maeneo ya Somalia na Ghuba ya Aden.
Wu aliongezea kusema kwamba kambi hiyo pia itasaidia kurahisisha harakati za vikosi vya kulinda amani katika kanda hiyo.
Vyanzo vya habari vya China vimetangaza kutiwa saini kwa mkataba wa miaka 10 kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya kutekeleza mpango huo.

Mwanzoni mwa mwezi Novemba, mkuu wa idara ya ulinzi ya China Fang Finghui pia aliwahi kutekeleza ziara ya Djibouti na kujadili suala la kuunda kambi inayotarajiwa kutumiwa na wanajeshi 10,000 wa China.

No comments: