Tuesday, 14 January 2014

200 wazama mto Nile huko sudan kusin

Waliofariki walikuwa watu waliokuwa wanatoroka vita Sudan Kusini
Zaidi ya watu 200 raia wa Sudan Kusini wamezama katika ajali ya boti kwenye mto Nile wakikimbia vita vinavyoendelea katika mji wa Malakal.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Sudan Kusini.

Boti hiyo iliyozama, ilikuwa imewabeba watu wengi kupindukia. Watu hao walikuwa wanatoroka vita vinavyotokota katika mji wa Malakal.

Mapigano yalizuka Sudan Kusini mwezi Disemba mwaka jana baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake wa Rais Riek Machar, kwa kuwa na njama ya kumpindua.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa tangu ghasia kuanza nchini humo.

Cristiano Ronaldo atunukiwa Ballon d'Or

Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa mwaka Ballon d'Or. Ujerumani ilinyakua tuzo tatu, wakati Jupp Heynckes na Silvia Neid wakishinda tuzo ya makocha bora


Nadine Angerer akiibuka mchezaji bora mwanamke. Katika sherehe za kila mwaka za Ballon d'Or mjini Zurich, Shirikisho la Soka Ulimwenguni - FIFA lilimtaja Cristiano Ronaldo kama mchezaji bora ulimwenguni katika msimu wa mwaka wa 2012/2013. Mreno huyo alipigiwa kura na kumpiku nyota wa Barcelona Muargentina Lionel Messi na Mfaransa Frank Ribery wa Bayern Munich. Kama Messi angeshinda, tuzo hiyo ingekuwa yake ya tano mfululizo.

“Namshukuru kila mmoja, wachezaji wenzangu, timu ya taifa na familia yangu, kila mtu hapa” alisema Ronaldo aliyebubujikwa machozi.

“Sina maneno mengine ya kuielezea hali hii” aliongeza. CR7 alishinda tuzo hiyo ya FIFA ya mchezaji bora ulimwenguni mara ya mwisho katika mwaka wa 2008.
Jupp Heynckes aliwabwaga Jurgen Klopp na Alex Ferguson kwa kunyakua tuzo ya kocha bora wa mwaka

Jupp Heynckes aliwabwaga Jurgen Klopp na Alex Ferguson kwa kunyakua tuzo ya kocha bora wa mwaka

Mfaransa Franck Ribery alipigiwa upatu kushinda tuzo hiyo, kufuatia jukumu lake alilotekeleza katika klabu yake ya Bayern Munich, kushinda taji la Bundesliga, DFB Pokal na Champions League katika msimu wa 2012/2013. Pia alinyakua tuzo ya Shirikisho la Soka Ulaya – UEFA, mchezaji bora wa msimu wa 2012/2013.

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi pia alikuwa kwenye orodha hiyo. Nyota huyo wa Barca alishinda mataji ya Ballon d'Or kwa miaka mitano mfululizo.

Ujerumani yashinda mataji matatu

Jupp Heynckes, kocha wa Bayern Munich katika msimu uliotangulia, alinyakua tuzo ya FIFA ya Kocha Bora wa Mwaka baada ya kuiongoza timu yake katika kutwaa mataji matatu.

Kocha mwenzake Mjerumani ambaye anaiongoza timu ya taifa ya wanawake Silvia Neid, alishinda tuzo hiyo kwa mara ya pili kwa upande wa wanawake. Aliishukuru FIFA kwa “kuitambua kandanda ya wanawake”.

Uwanjani katika soka la wanawake, mlinda lango wa Ujerumani na nahodha wa timu ya taifa Nadine Angerer, ambaye ni mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya, alimpiku Mbrazil Marta na Abby Wambach wa timu ya taifa ya Marekani

Mbunge Ndesamburo ajitosa kumtetea Lowassa

Edward Lowasa,(kulia) akibadilshana mawazo na Wabunge wa Chadema
Kocha wa City alimlaumu refa kwa kukosa kumuadhibu Yanga-Mbiwa aliyemjeruhi Nasri






Mchezaji wa kiungo cha kati, wa Manchester City Samir Nasri, atafanyiwa uchunguzi zaidi wa jereha la goti alilopata wakati wa mechi ya klabu hiyo dhidi ya Newcastle.

Nasri aliondoshwa uwanjani baada ya kufanyiwa masihara na Mapou Yanga wakati wa mechi yao ambapo walishinda mabao mawili kwa nunge

Kocha wa City Manuel Pellegrini alighadhabishwa mno na tukio hilo na kusema kuwa mtu aliyepaswa kuadhibiwa ni Yanga-Mbiwa.

"Nasri amepata jeraha baya sana. Ilipaswa kuwa kadi nyekundu kwa Yanga,'' alisema Pellegrini

"alijeruhiwa vibaya lakini tutajua hali yake Jumatatu,'' aliongeza kusema kocha huyo.

Meneja wa Newcastle hata hivyo alimtetea Yanga-Mbiwa.

"haikuwa nia yake kumjeruhi Nasri," alsema kocha Pardew. " hiyo sio kawaida yake na natumai kuwa Nasri yuko salama.''

Nasri ambaye huchezea timu ya kitaifa ya Ufaransa, aliondoka uwanjani dakika ya 79 na kupokea matibabu kwa dakika chache, kabla ya kuondoka akiwa analia kwa uchungu

Yanga-Mbiwa hata hivyo alipata onyo la refa.

Kocha Pellegrini pia alithibitisha kuwa Edin Dzeko, aliyeingiza bao lililowapa ushindi City na kuwaweka katika nafasi ya kwanza katika ligi ya premier, alipata jeraha la mguu
Muumini wa Dini ya Kiislam Mohamad Abdulkadir, akipamba taa kwenye msikiti wa Faizan-E-Madina kwa ajili ya mkesha wa Sikukuu ya Maulid inayofanyika leo


Waumini mbalimbali wa dini ya Kiislamu nchini, wanaungana na wenzao duniani kote leo katika mapumziko ya kuadhimisha Sikukuu ya Maulid ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) miaka 1345 iliyopita.

Msemaji wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Shaaban Simba alisema jana kuwa, kitaifa Maulid hayo yalifanyika jana usiku mkoani Kigoma.

Alisema Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba ndiye aliyeongoza Maulid hayo kitaifa na mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa huo, Issa Machibya.

Simba alitumia fursa hiyo kuwatakiwa Watanzania wote mapumziko mema ya Maulid kwa kusherehekea kwa amani na kuepuka kujihusisha na vitendo viovu.

“Tunawaomba wananchi kutumia mapumziko haya vizuri kwa lengo la kulinda amani na utulivu wa nchi yetu,” alisema Simba. Jijini Dar es Salaam, maadhimisho hayo yalifanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.

Sunday, 12 January 2014

Kamati ya Maadili CCM yatakiwa kuwashughulikia waliotangaza nia

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Philiph Mangula


Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umeshauri Kamati ya Maadili ya CCM kuwaonyesha mlango wa kutokea wote walioanza kampeni za kugombea urais, ubunge na nyingine kinyume cha maadili ya chama.

Umesema wagombea hao ambao umewaita wasio rasmi, wameonywa mara kadhaa na viongozi wa chama ikiwamo kupitia kwenye vyombo vya habari, lakini wameshindwa kujitambua na kujirekebisha.

UVCCM umedai wagombea hao wasio rasmi katika kampeni zao tayari wameanza kusababisha kutoweka kwa mshikamano ndani ya chama, kwani wamekuwa wakipita nchi nzima kushawishi kwa fedha na rushwa nyingine mbalimbali makundi ya jamii ili kuungwa mkono.

Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Taifa, Paul Makonda alisema Kamati ya Maadili ya CCM ina wajibu wa kutafsiri hasira ya wanaCCM dhidi ya kampeni hizo ambazo zinakijeli chama, uongozi wa nchi uliopo na kuleta nyufa.

“Tunachokiona sasa ni tofauti kabisa na malezi na makuzi yetu ndani ya chama, kwani tayari baadhi ya wanaCCM bila uoga wala aibu wameshajitangaza ni wagombea urais, ubunge, udiwani na nafasi nyingine za kupigiwa kura, wameanza kampeni za kishindo za rushwa na vishawishi mbalimbali nje kabisa ya utaratibu, kanuni na maadili ya chama,” alisema Makonda na kuongeza:

“Watu hawa waonyeshwe mlango wa kutokea, tusipoziba ufa huu sasa tujiandae kujenga ukuta mwakani kwa gharama kubwa kupindukia.”

Makonda alisema kwa sababu mwaka huu kuna mchakato wa chaguzi mbalimbali zitakazohitimishwa mwakani na ushaguzi mkuu, mshikimamo wa hali ya juu unahitajika ndani ya chama.

“Kwa sasa ilani ya CCM ya mwaka 2010 imewekwa pembeni, kinachonadiwa ni ilani binafsi za kumwaga fedha nchi nzima, kusambaza elimu kama njugu, bila kueleza vyanzo vya mapato ya Serikali zao za kusadikika,” alisema. Alisema hatua hiyo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za chini, maadili, miiko ya chama.

pamoja na Serikali kwa ujumla ambapo ipo wima katika kuhakikisha kuwa ilani ya CCM ya mwaka 2010 inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Alisema CCM inataratibu zake za kupata viongozi na wote tunazijua, kufanya kinyume na taratibu hizi ni uasi, upungufu wa busara, na ukosefu wa sifa ya uongozi.

“ Hivyo vijana wa CCM tunamuunga mkono Mwenyekiti wa CCM taifa Dk Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti, Philiph Mangula na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama Nape Nnauye waliokemea tabia hii mpya hatarishi kwa chama chetu ya kuhaha kupata uongozi nje ya taratibu na kutumia vishawishi vyenye sura ya rushwa vitakavyokitia doa chama,”

Makonda alisema kuwa maadili na kanuni za chama ni kuwaunganisha wanaCCM wote kuwa kitu kimoja, hivyo dalili zozote nje ya tunu hizo ni usaliti, uasi ambao hauna budi kupigwa vita kwa nguvu zote kwa vijana.