Riyad Mahrez ameruhusiwa kuondoka
katika kambi ya kikosi cha Algeria na kurudi Ulaya ili kukamilisha
uhamisho wake hadi klabu mpya kulingana na shirikisho la soka nchini
Algeria.
Winga huyo wa Leicester aliwasilisha ombi la kutaka
kuondoka katika uwanja wa King Power na amehusishwa na vilabu vingi huku
Roma ikiwa tayari imewasilisha ombi la kumununua mchezaji huyo mara
tatu , ombi la mwisho likiwa lile la dau la £32m.Thursday, 31 August 2017
Monday, 14 August 2017
Waziri Mkuu aagiza wananchi wasizuiwe kuonyesha mabango
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ametaka mabango yanayoonyeshwa na wananchi kwa
viongozi wa kitaifa wanapowatembelea yasiwe yanazuiwa kwa vile yanakuwa
yanaelezea changamoto wanazokabiliana nazo.
Majaliwa alisema hayo baada ya kuona mabango yaliyoinuliwa na wananchi kwenye mkutano wake na wananchi mwishoni mwa juma lililopita mjini Sikonge mkoani Tabora huku wananchi hao wakitakiwa kuyashusha.
“Siku nyingine msirudie na kuanzia sasa waacheni wananchi waonyeshe mabango yao kwani ndiyo njia wanayotumia kuonyesha hisia zao kwa yale wanayokumbana nayo na kuwasababishia kero,” alisema Majaliwa.

Subscribe to:
Posts (Atom)