Thursday, 23 April 2015

Manchester kumchukua Hammels kwa paund milion 30

over

Manchester United imeshaanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao baada ya msimu huu kuelekea mwishoni. Kiasi cha €30 million zimetengwa kwa ajili ya kumnasa mkali huyu.


Kwa muda sasa hivi Man United wamekua imehusishwa na uhamisho wa Hummels. Hummels ambae alionekana kuwa ni defender bora kwenye kombe la dunia anaonekana ni mmoja kati ya mastaa wanatarajiwa kusepa Borussia Dortmund.


Kutokana na kocha Jurgen Klopp kutangaza kusepa mwishoni mwa msimu huu basi kuna mwanya mkubwa wa mastaa wa timu hiyo kusepa pia.


Kiasi cha €30 million kimetolewa kama offer ya kwanza kumnasa Mats Hummeles ana miaka 26, amecheza mechi 181 tangu asajiliwe rasmi na Borussia na amefunga magoli 16 akicheza nafasi ya Center defender.

Ajali nyingine shinyanga yaua 10 na 50 kujeruhiwa

Polisi wakiwa katika eneo la Ajali
Jinamizi la ajali za barabarani zikihusisha mabasi zimeendelea kugharimu maisha ya Watanzania baada ya jana watu 10 kupoteza maisha na wengine 50 kujeruhiwa vibaya wakati basi la Unique Express lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Tabora kugongana uso kwa uso na lori la Coca-Cola lililokuwa likitokea Tinde kuelekea Shinyanga.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 8.45 mchana katika Kijiji cha Ibingo, Kata ya Samuye, Shinyanga.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la tukio, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi uliosababisha dereva wake kushindwa kulikwepa lori hilo lililokuwa katikati ya barabara.
Alisema watu tisa walifariki dunia papohapo na mmoja alifia katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga akipatiwa matibabu.
Kamanda Kamugisha alisema dereva wa lori anashikiliwa na polisi mwenzake wa basi hali yake ni mbaya na amelazwa hospitali.
Alisema wengi waliofariki dunia walikuwa wamekandamizwa na vyuma hali iliyowalazimu kuomba msaada wa winchi kuliinua basi hilo na kuwatoa.
Kamanda Kamugisha aliwataka wananchi na abiria kutoa taarifa pindi wanapoona madereva wakiendesha mwendo ambao unaweza kuhatarisha maisha yao.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo akiwamo Diwani wa Kata ya Samuye, Amos Shija walisema walishtushwa na kishindo cha kugongana kilichofuatiwa na kelele na vilio vya abiria.
Shuhuda, John Bundala aliitaka Serikali kuendelea kuwachukulia hatua kali madereva ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani na kupoteza maisha ya watu wasiokuwa na hatia na wengine kupata ulemavu.

Timu Nne zatinga nusu fainali UEFA

Javier Hernandez akishangilia goli mbele ya mashabiki wa Real Madrid
Timu nne zimetinga hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyokamilika hapo jana, baada ya Real Madrid ya Hispania na Juventus ya Uitaliano kufanikiwa kuingia nusu fainali.

Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu, Madrid walilazimika kusubiri hadi dakika ya 88, walipopata bao lao la pekee lililotiwa kimia Javier Hernandez almaarufu kama Chicharito,na hivyo kuhitimisha safari ya Atletico Madrid.
Katika msimu uliopita, huko Lisbon Ureno, Atletico walitolewa na Real Madrid katika hatua ya fainali.
Nayo Juventus imezima matumaini ya Monaco ya Ufaransa kwa kulinda bao lake lililofungwa katika mechi ya awali na hapo matokeo ikawa sare ya bila kutofungana. Hata hivyo nyota ni njema kwa Spain ambao sasa wanawakilishwa na timu mbili ambazo ni Real Madrid na Barcelona.

Monday, 20 April 2015

Lowasa amshinikiza Kikwete asaini kunyongwa kwa wauaji wa maalbino

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameitaka jumuiya ya albino nchini kuisukuma Serikali ili Rais Jakaya Kikwete asaini utekelezaji wa hukumu ya kuwanyonga wauaji wa albino.
Kauli ya Lowassa imekuja wiki moja tu baada ya Rais Kikwete kusema hajapelekewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya albino kutokana na mlolongo mrefu wa kisheria uliopo kabla ya kumfikia.
Rais Kikwete alisema hayo wakati wa ibada maalumu ya kuwekwa wakfu Askofu Liberatus Sangu kuwa Mhashamu Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga.
Hata hivyo, jana Lowassa aliyekuwa mgeni rasmi katika kampeni ya matembezi kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yaliyoandaliwa na Klabu za Mbio za Pole ya Temeke na kushirikisha vikundi mbalimbali vya Dar es Salaam, alisema: “Ninampongeza Rais Kikwete kutokana na jitihada zake za kukemea mauaji ya albino. Pia, nimesikia kuna watu sita wametakiwa kunyongwa lakini kwa maelezo ya Rais hukumu hizo hazijamfikia, hivyo nawaomba mfanye msukumo ili Rais asaini.”
Kutokana na kukithiri mauaji hayo, Lowassa aliiomba Serikali kuunda kamati maalumu itakayokuwa ikichunguza mauaji ya walemavu hao bila kutegemea kamati za mikoa ili kuongeza ufanisi wa kuilinda jamii hiyo.
Mwanasiasa huyo anayetajwa kutaka kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, aliuambia umati uliokusanyika katika viwanja vya TCC Chang’ombe kuwa suala la ulinzi wa albino si la Serikali pekee bali la wananchi wote.
Mapema Machi mwaka huu, Mahakama Kuu ya Tanzania iliwahukumu watu wanne kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na kosa la kumuua Zawadi Magindu (32) mwenye ulemavu wa ngozi, mkazi wa Kijiji cha Nyamaruru, Wilaya ya Geita.
Kifungo cha CCM
Awali wakati akitoa hotuba yake Lowassa alisema kutokana na kifungo alichowekewa na CCM hawezi kuzungumza mambo mengi kwa sababu yatamletea balaa.
“Kule CCM bado nina kifungo, nikisema mengi nitaleta balaa,” alisema huku akishangiliwa na kundi la vijana waliokuwapo uwanjani hapo.
Lowassa yupo kifungoni na makada wengine watano ambao ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Mbunge wa Sengerema William Ngeleja, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wasira na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Aliyekuwa mbunge wa Temeke (CCM), John Kibaso alisema Lowassa alikubali kuwa mgeni rasmi baada ya kumuomba aridhie ombi hilo kutokana na mambo yake ya kisiasa yanayomkabili.
“Awali mgeni rasmi ilibidi awe mbunge wa Ilala, Mussa Zungu lakini ikabidi tumuombe Lowassa aliyetuambia kuwa anaogopa CCM kwa kuwa haijaruhusu mambo hayo.
Hata hivyo, ndani ya wiki moja mzee wetu alikubali kushiriki nasi kama mlivyomuona,” alisema Kibaso.
Katika maandamano hayo Lowassa aliviongoza vikundi mbalimbali vya mbio za pole katika matembezi ya haraka kutoka Uwanja wa Taifa hadi viwanja vya TCC Chang’ombe.
Pia aliongozana na Mbunge wa Temeke (CCM) Abbas Mtemvu, Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan na Zungu.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye albino Tanzania (TAS), Ernest Kimaya alisema ukataji wa viungo na kuuawa kwa watu wenye ualbino umetia doa nchi jambo ambalo linapaswa kukemewa na wadau mbalimbali.
Alisema mauaji hayo yameongezeka kwa kasi kuanzia mwaka 2006 ambapo hadi sasa watu wenye ulemavu huo wameuawa 75, waliojeruhiwa kwa kukatwa viungo ni 35 na makaburi 15 yalifukuliwa na kuchukuliwa viungo vya mwili.

Aston Villa yaapa kuinyanganya Arsenal Kombe la FA

Tim Sherwood kocha wa Aston Villa aipania Arsenal

Arsene Wenger
Baada ya Aston Villa kushinda bao 2-1 dhidi ya Liverpool katika mechi ya nusu Fainali michuano ya FA Cup,sasa kocha wa Aston Villa Tim Sherwood anasema wanajinoa kuwakabili Arsenal katika mechi ya fainali.
Hata hivyo amesema kuwa wanatakiwa kujiandaa vilivyo kwani Arsenal katika mechi za awali walizocheza nao waliwahi walipewa kipigo cha 3-0 na 5-0 hivyo akasema maandalizi wanayopaswa kuyafanya si ya mzaha.
Sherwood amesema kuwa kuna kazi kubwa ya kufanyika ya maandalizi kuanzia sasa hadi siku ya May,30mwaka huu.
Tutakachotakiwa kukifanya nikujilinda,lakini wakati huo huo kushambulia na kuhakikisha tunawashinda Arsernal.

Chadema yamtangaza Zitto kama adui namba moja wa chama hicho

MNYIKACHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuwa adui yake namba moja ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and Transparance (ACT-wazalendo), Zitto Kabwe.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha Mwanza juzi, alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutokana na kile alichosema ‘ni adui kwao’.
“Mtume Muhamad (S.A.W) alikuwa anazungumzia unafiki ambao una sura mbili na sifa zake, leo (ACT) wanasema wapo upinzani, wanasema msiunge mkono Ukawa halafu mnawakaribisha?
“Nendeni kila mahali waambieni wananchi adui yetu mkuu ni Zitto. Sikilizeni niwaambie Taifa hili kama ni ufisadi tumeshazungumzia sana kuanzia EPA mpaka Richmond. Dk. Slaa (Willbrod) alipoingia bungeni aliyasema haya kwa sasa si mapya. Adui yetu ni Zitto na hatumtaki Ukawa,” alisema Mnyika.
Alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo Ukawa kwa sababu adui kwao.
Zitto ajibu
Akihutubia mamia ya wananchi wa Mwanza jana, Zitto alisema kadri siku zinavyosonga wabaya wake wamekuwa wakijionyesha.
Zitto alisema pamoja na hali hiyo, ACT-Wazalendo haiko tayari kuzungumzia siasa za wakati uliopita kwa vile kufanya hivyo si afya njema kwa siasa za upinzani.
Alisema ni vema viongozi wa vyama vya upinzani waachane na ugomvi binafsi na watangulize masilahi ya taifa mbele.
“Mwanzo walipotufukuza walituambia tukatafute vyama vingine hilo likafanyika, tulipopata vyama vya kufanyia siasa wakasema vipo kwa ajili ya kugawa upinzani tukasema tupo tayari kuunganisha nguvu ya pamoja kwa ajili ya kuiondoa CCM…wenzetu pia hili hawalitaki sasa ni wajibu wenu kutambua watu gani hawataki kuiondoa CCM,” alisema Zitto.
Alisema wao (ACT) wana nia ya dhati lakini wenzao wanaweka ugomvi binafsi mbele ya masilahi ya taifa.
“Sisi ACT Wazalendo bado tupo tayari kushirikiana kwa mujibu wa misingi. Shabaha yetu ni moja tu, kubomoa mfumo wa uchumi wa kinyonyaji na ufisadi ili kujenga uchumi shirikishi wa wananchi,” alisema na kuongeza:
“Sikufundishwa kugombana na watu barabarani au kusema ovyo mitaani, kufanya hivi hakuna tofauti na kumsema mke au mume mlioachana…mmoja kwa kukosa busara na kwa kuwa aliachana na yule mke anaamua kwenda vijiweni na kutoa siri za mzazi mwenzie, hili kwetu hapana.
“Tunakuja na jahazi jipya ambalo ndugu zangu wa Mwanza nimekuja kuwakabidhi, kubwa tunataka kulirudisha taifa katika misingi yake ya ujamaa na kujitegemea, tunahitaji ujamaa wa demokrasia,” alisema Zitto.
Alisema tafsiri ya ujamaa haina maana kuwa chama hicho kitataifisha mali za watu, bali kitarekebisha makosa ya ubinafsishaji kwa kurejesha mali zote za taifa zilizouzwa na wanunuzi hawajatekeleza mikataba yao.
Mapokezi
Zitto ambaye amefuatana na Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira, waliwasili Mwanza saa 8.00 mchana na kupata mapokezi makubwa yaliyoanzia wilayani Misungwi.
Mapokezi hayo yaliongozwa na vijana waendesha pikipiki (bodaboda) na kikundi cha wanawake ambao muda wote walikuwa katika shamrashara hadi alipoingia kwenye uwanja wa Furahisha.

Friday, 3 April 2015

Wakenya wapewa amri ya kutotoka nje kwa Wiki mbili

Serikali imetoa amri ya kutotoka nje Garissa Kenya
Serikali ya Kenya imetangaza amri ya kutotoka nje usiku kwa muda wa wiki mbili katika kaunti kadhaa kaskazini mashariki mwa Kenya.
Amri hiyo iliyotolewa na mkuu wa polisi nchini humo, imetolewa baada ya wanamgambo wa kundi la Al shabaab lenye makao yake nchini Somalia kuwaua zaidi ya watu 147.
Mbunge wa eneo hilo, ambaye pia ni kinara mkuu wa upande wa wanasiasa wengi bungeni, Aden Bare Duale, ameiambia BBC kuwa Waziri wa maswala ya ndani ya taifa anafanya mkutano wa dharura wa usalama mjini Garissa.
Serikali imetoa zawadi nono kwa mtu atakayetoa ripoti ya kukamatwa kwa mhusika mkuu katika shambulio hilo.