Sunday, 10 January 2016

Mwanamke nchini Kenya achomwa kisu usoni na mume wake

Mwanamke nchini Kenya achomwa kisu usoni na mume wakeMwanamume mmoja nchini Kenya afikishwa mahakamani kwa kumchoma kisu cha usoni mke wake

Wakenya watoa wito wa kufanyika hatua za haraka, baada ya mwanamume mmoja aliyefikishwa mahakamani kwa kosa la kumchoma kisu mke wake chenye urefu wa nchi 10 usoni ambapo ilibidi kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kuondolewa,lakini mwanamke huyo amekataa kutoa ushahidi dhidi ya mumewe.
Kesi hiyo imeonekana kusambazwa mno katika mitandao ya twitter katika nchi za Afrika mashariki ambapo kumekuwa na unyanyasi mwingi wa wanawake huku watuhumiwa kutopata adhabu yoyote.
Picha nyingi zinazomuonyesha mwanamke huyo akiwa amechomwa kisu katika shavu na pia picha za X-ray zikionyesha kisu kimeingia upande wa kulia na kuchomoza hadi upande wa pili zimesambazwa katika mitandao ya kijamii huku zikiwa na maandishi yanayosema “haki kwa Fatuma”.
Mkurugenzi wa mashtaka alisema katika taarifa yake Twitter, kuwa Bwana Mohamed Deeq alikanusha kosa lake la kumchoma kisu mkewe Fatuma Ibrahim,wakati wa ugomvi wao wa ndani katika mahakama iliyopo katika mkoa wa Wajir kaskazini mashariki mwa Kenya siku ya Ijumaa.
Kaimu naibu wa DPP Nicholas Mutuku,aliiambia Reuters kuwa Deeq bado anashikiliwa katika  kituo cha polisi mkoani Wajir mpaka atakapo shitakiwa tarehe 13 januari.

Saturday, 9 January 2016

Zitto: Rais Magufuli Ameshaipotezea Nchi Mapato ya Bilioni 8 Tangu Aingie Madarakani

Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ameilalamikia serikali ya Magufuli kwa kitendo chake cha kukaa kimya kuhusu ufisadi unaoendelea kufanywa na Harbinder Singh Seth, mmiliki wa IPTL, ambaye huvuna kiasi cha malipo ya bilioni 4 kila mwezi kama malipo ya kuliuzia umeme shirika la ugavi wa umeme nchini, Tanesco.

Zitto ambaye ni mmoja wa wabunge walioibua na kusimamia kidete sakata la ufisadi wa Tegeta Escrow bungeni mwishoni mwa mwaka juzi (2014), amesema hayo kufuatia tangazo la serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support ya miaka ya miaka 1980 na 1990s, ambapo ameisifu serikali kwa hatua hiyo na kuhoji iweje ikomae na kashfa hiyo tu, huku ikisita kuchukua hatua kwenye sakata la IPTL linaloigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha kila mwezi isivyostahili?

Kampuni ya IPTL imeshalipwa fedha mara mbili tangu Rais Magufuli aingie rasmi madarakani, hivyo kufanya hesabu zitimie bilioni 8 kwa kipindi cha miezi miwili mpaka sasa.

Msome;

"Nimeona tangazo la Serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support. Hii ni kashfa ya miaka ya 1980s na 1990s. Ni hatua nzuri. Lakini ina maana gani wakati Serikali inavuta miguu kwenye suala la IPTL? Harbinder Singh Seth na genge lake wanavuta tshs 4bn kila mwezi. Kwa kutochukua hatua kuhusu IPTL, Rais Magufuli ameshaipotezea nchi mapato ya tshs 8bn tangu aingie madarakani. ‪#‎TegetaEscrow‬ ndio baba la mtandao wa ufisadi nchini kwetu" - Zitto Kabwe.

Adele aiba wimbo wa msanii maarufu Ahmet Kaya wa Uturuki

Adele aiba wimbo wa msanii maarufu wa UturukiAdele aiba wimbo wa msanii maarufu Ahmet Kaya wa Uturuki

Hakuna tena shaka muimbaji Adele kutoka Uingereza imebainishwa kuwa alitumia wimbo wa msanii maarufu wa zamani wa Uturuki aliekuwa akitambulika katika ulimwengu wa muziki kwa ina la Ahmet Kaya.
Wimbo ambao Adele aliiba si mwingine ni wimbo uliotoka kwa jina la "Acilara Tutunmak".
Wimbo huo Adele aliubadilisha jina na kutengeneza kibao chake cha "Million Years Ago" ambacho kinafanya vizuri katika soko la muziki.
Kufanana kwa nyimbo hizo mbili kumeleta gumzo katika ulimwengu wa muziki.
Iwapo mke wa Ahmet Kaya, Bi Gulten Kaya anaweza kukata rufaa mbele ya vyombo vya sheria kuhusu wimbo huo.

Mtuhumiwa namba Moja Kesi Ya Mauaji ya Dk. Mvungi Afariki

Mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dk. Sengondo Mvungi ameripotiwa kufariki akiwa gerezani, siku chache kabla ya kesi kusikilizwa.
Taarifa ya kifo cha mshtakiwa huyo aliyetajwa kwa jina la Chibago Chiuguta mwenye umri wa miaka 33, zilitolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kueleza kuwa mshitakiwa huyo alikutwa akiwa amekutwa na umauti.
Kufuatia taarifa hizo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Thomas Simba aliagiza upande wa Magereza kuhakikisha wanafuatilia cheti cha kifo cha mshitakiwa huyo.
Marehemu alikuwa kati ya washtakiwa 11 waliodaiwa kumuua Dk. Mvungi katika eneo la Msakuzi, Kiswegere katika wilaya ya Kinondoni. Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya kosa hilo Novemba 3 mwaka 2013.
Upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.

Friday, 8 January 2016

Mwanachama wa IS amuua mamake hadharani

ISKundi la IS hutekeleza sheria kali za Kiislamu
Mpiganaji wa kundi la Islamic State nchini Syria amemuua mamake hadharani kwa sababu alimwambia ahame kundi hilo, wanaharakati wanasema.
Ali Saqr, 21, alimuua mamake, Lena al-Qasem, 45, nje ya afisi ya posta mjini Raqqa, Syria, watu walioshuhudia wanasema.
Mji wa Raqqa umekuwa ukihudumu kama mji mkuu wa IS tangu wapiganaji hao kutekwa mji huo Agosti 2013.
Kundi hilo huwa halivumilii watu wanaopinga msimamo wake na kutoa adhabu kali kwa wanaopinga kundi hilo, na mara nyingi adhabu hutekelezwa hadharani.
Maafisa wa Shirika la Syrian Observatory for Human Rights (SOHR) lenye makao yake Uingereza na kundi la wanaharakati wa Raqqa is Being Slaughtered Silently (Raqqa Inachinjwa Kimy akimya) wamethibitisha kisa hicho.
Lena al-Qasem alikuwa amemwambia mwanawe kwamba muungano unaoongozwa na Marekani ungeangamiza kundi hilo, na akajaribu kumshawishi ahame mji huo pamoja naye.
Mwanawe alijulisha wenzake katika IS, na agizo likatolewa auawe.
Ali Saqr anadaiwa kumpiga risasi mamake nye ya afisi ya posta mbele ya mamia ya watu.
Kundi la IS hutekeleza sheria kali za Kiislamu, zenye kuegemea madhehebu ya Kisuni.
Kundi hilo limedhibiti maeneo ya Iraq na Syria tangu 2014

Thursday, 7 January 2016

Messi aing’arisha Barcelona

MessiMessi alifungia Barca mabao mawili
Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amekuwa shujaa baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Espanyol katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe la Mfalme, maarufu kama Copa del Rey.
Mechi hiyo ilichezewa uwanja wa Nou Camp.
Katika ushindi wa mabao hayo manne wachezaji wengine walioiwezesha timu hiyo kushinda ni Gerard Pique na Neymar Da silva.
Bao pekee la Espanyol lilifungwa na Felipe Caicedo.
Espanyol walimaliza mechi hiyo wakiwa na wachezaji tisa uwanjani baada ya Arsensio Pérez na Diop kuonyeshwa kadi nyekundu.
Kufuatia mabao hayo, Messi sasa amefikisha idadi ya mabao aliyofunga msimu huu, licha ya majeraha, hadi 14 kutoka kwa mechi 21.
Messi ni mmoja wa wanaoshindania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani ijulikanayo kama Ballon d'Or. Mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa Jumatatu wiki ijayo.

Wednesday, 6 January 2016

Polisi wakamata silaha kadhaa nchini Kenya

Polisi wakamata silaha kadhaa nchini KenyaSilaha kadhaa zakamatwa kwenye nyumbani moja ya mshukiwa wa ugaidi mjini Mombasa

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamekamata silaha kadhaa baada ya kuvamia nyumba moja ya mshukiwa wa ugaidi iliyoko mjini Mombasa.
Silaha hizo zilizokamatwa zilikuwa ni bunduki aina ya G3 na risasi zake 20, bunduki aina ya M4 na risasi zake 7, pamoja na risasi nyingine 318 za ziada.
Wakati huo huo, kompyuta moja na simu 15 za rununu pia zilipatikana kwenye nyumba hiyo.
Silaha na vifaa hivyo vya mawasiliano vinadaiwa kupangwa kutumika katika utekelezaji wa mashambulizi ya kigaidi mjini humo