Kesi hiyo imeonekana kusambazwa mno katika mitandao ya twitter katika nchi za Afrika mashariki ambapo kumekuwa na unyanyasi mwingi wa wanawake huku watuhumiwa kutopata adhabu yoyote.
Picha nyingi zinazomuonyesha mwanamke huyo akiwa amechomwa kisu katika shavu na pia picha za X-ray zikionyesha kisu kimeingia upande wa kulia na kuchomoza hadi upande wa pili zimesambazwa katika mitandao ya kijamii huku zikiwa na maandishi yanayosema “haki kwa Fatuma”.
Mkurugenzi wa mashtaka alisema katika taarifa yake Twitter, kuwa Bwana Mohamed Deeq alikanusha kosa lake la kumchoma kisu mkewe Fatuma Ibrahim,wakati wa ugomvi wao wa ndani katika mahakama iliyopo katika mkoa wa Wajir kaskazini mashariki mwa Kenya siku ya Ijumaa.
Kaimu naibu wa DPP Nicholas Mutuku,aliiambia Reuters kuwa Deeq bado anashikiliwa katika kituo cha polisi mkoani Wajir mpaka atakapo shitakiwa tarehe 13 januari.
No comments:
Post a Comment