Monday 4 January 2016

TETESI ZA SOKA ULAYA

Manchester United wanajiandaa kutoa pauni milioni 140, ili kutengua kigezo cha uhamisho cha Neymar, 23 anayeichezea Barcelona, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua (Le Sport10), Manchester United watamruhusu kiungo wao Nick Powell, 21 kwenda kwa mkopo katika timu moja ya ligi daraja la kwanza (Sun), Southampton hawatomuuza Sadio Mane, 23 au Victor Wanyama, 24 katika dirisha la usajili ya Januari (Times),

Liverpool wanatarajiwa kutangaza kumsajili kiungo kutoka Seria Marko Grujic, 19, anayechezea Red Star Belgrade (Sky Sports), Kolo Toure, 34, ambaye mkataba wake na Liverpool unamalizika mwisho wa msimu huu anasakwa na Lazio ya Italia (II Messaggero), meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema klabu yake itafanya usajili ndani ya siku 10 zijazo (Talksport), Arsenal wameambiwa na Bayer Leverkusen wasahau kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez, 27 (Sun), Newcastle United wana matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa QPR Charlie Austin, 26, kufuatia kuumia kwa Papiss Cisse ambaye atakuwa nje kwa miezi mitatu (Daily Mail), beki wa Serbia na Chelsea, Branislav Ivanovic, 31, anasakwa na AC Milan na pia Inter Milan (Daily Mirror), Arsenal hawafanyi mazungumzo yoyote na mshambuliaji wa Dinamo Moscow Aleksandr Kokorin (Sports), mshambuliaji wa Locomotiv Moscow, Oumar Niasse anajiandaa kuhamia England kwa pauni milioni 15, huku Manchester United, Chelsea na Tottenham wakimfuatilia (Guardian), Chelsea wanafikiria kumchukua kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Partey (Caughtoffside), Chelsea pia wanafikiria kumwania Isco, anayesakwa na Manchester City na Juventus. Chelsea vilevile wameanza mazungumzo na Alex Teixeira kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 30 kutoka Shaktar Donetsk (Evening Standard), AC Milan wanataka kumsajili Maroanne Fellaini kwa mkopo kutoka Manchester United (Corriere della Sera), West Ham wameungana na Everton na Totenham kumsaka kiungo wa AC MIlan Keisuke Honda (Tuttosport). Uhamisho uliokamilika nitakujuza ukithibitishwa.

No comments: