Hatimaye baada ya danadana za muda mrefu, uchaguzi wa
kuwachagua Mameya wa Manispaa za Kinondoni na Ilala, umefanyika na Umoja
wa Vyama vinavyunda Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamefanikiwa kuongoza
Manispaa hizo.
Chaguzi hizo zilizhairishwa mara mbili kutokana na mvutano
uliotokewa katika chaguzi za nyuma, ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kwa
amri za mahakama.
Kwa upande wa Manispaa ya Kinondoni,Diwani wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, Boniface Jacob amefanikiwa kuwa Meya wa manispaa hiyo baada ya kushinda kwa kura 38 dhidi ya mpinzani wake, Benjamin Sitta wa CCM aliyepatakura 20. Naibu Meya ni Diwani wa Tandale kwa tiketi ya CUF, Jumanne Ameir Mbunju.
Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala leo pia uliingia katika
mgogoro kati ya madiwani wa CCM na wale wa Ukawa, hali iliyosababisha
CCM kususia uchaguzi huo na kuwaacha Ukawa kupiga kura peke yao na
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kumtangaza Charles Kuyeko (Chadema)kuwa
mshindi wa kiti cha Meya wa Ilala kwa ushindi wa kura 31, wakati Naibu
Meya ni Omary Kumbilyamoto (CUF) ambaye amepata kura 31.
Jumla ya madiwani waliotakiwa kupiga kura katika uchaguzi
huo ni 54, hivyo madiwani 31 wa Ukawa waliobaki ndani walitimiza akidi
ya uchaguzi huo kuendelea.
No comments:
Post a Comment