Mshambuliaji wa
timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana
Samatta leo hii anatarajiwa kuwasili nchini Nigeria kuhudhuria sherehe
za utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora barani Afrika zitakazofanyika
katika mji wa Abuja Alhamisi tarehe 7 Januari.
Mbwana Samatta
anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, huku
pia akiwa mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa (CAF CL) baada
ya kuifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao 8 na kuibuka mabingwa wapya
wa michuano hiyo.Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika pamoja na mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba (Congo DR) na mshambuliaji wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah (Algeria).
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameandamana na Samatta kuhudhuria sherehe hizo.
No comments:
Post a Comment