Korea Kaskazini
inasema kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya majaribio ya bomu la
nguvu ya maji, maarufu kama bomu la haidrojeni.
Tangazo hili
limetolewa na runinga ya taifa baada ya kusikika mitetemeko ya ardhi ya
kipimo cha tano nukta moja, karibu na eneo kuliko na kinu cha nyukilia.
Wataalamu wa Marekani wanafanya uchunguzi ikiwa yalikua majaribio ya
bomu hilo au ilikua zana nyingine ya nyuklia isiyokuwa na nguvu.Mwandishi wa BBC anasema bomu la nguvu ya maji lina uwezo mkubwa wa mlipuko ikilinganishwa na mabomu mengine yenye madini ya Plutonia ambayo Korea kaskazini imefanya majaribio katika miaka ya awali.
Mamkala za Pyongyang zimefanyia majaribio mengine matatu ya kinyukilia katika eneo kulikofanywa majaribio ya sasa kwa kipindi cha miaka kumi
No comments:
Post a Comment