Tuesday 12 January 2016

Messi atwaa tuzo ya Balloon D'or

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona, na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, ametwaa tuzo ya mchezo bora wa dunia.
Messi mwenye miaka 28 alishinda kwa 41.33% kwa kura zote zilizopigwa, huku Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa 27.76% na Neymer akipata 7.86%.
Hii ni mara yake ya tano kutwaa tuzo hiyo.
Kwa upande wa wanawake nyota wa Marekani Carli Lloyd, ameibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake.
Goli bora la mwaka likifahamika kama Puskas limwendea Wendell Lira anayekipiga katika Atletico Goianiense ya Brazil.
Kocha wa Barcelona Muhispania Luis Enrique amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa kuiongoza barca kufanya vizuri barani Ulaya kwa kutwa mataji matano msimu uliopita.
Jill Ellis kocha wa kikosi cha taifa cha Marekani amekuwa kocha bora wa wanawake baada ya kuongoza timu ya taifa ya Marekani kufanya vyema katika michuano ya kombe la dunia.

No comments: