 |
| Magufuli apunguza kodi ya mapato na 2%
|
Huku wafanyikazi kote duniani wakiadhimisha sikukuu ya wafanyakazi, nchini Tanzania, wafanyikazi wanakila sababu ya kutabasamu.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewaongezea wafanyikazi wote nchini humo asilimia mia mbili 2% mishahara.
Katika
hotuba ya kuadhimisha siku ya wafanyikazi, bw Magufuli alitangaza
kupunguzwa kwa kodi ya mapato PAYE kutoka asilimia 11% hadi asilimia 9%.
Hii inamaanisha kuwa kila mfanyikazi atapata ongezeko la mapato yake kwa asilimia 2%.
Magufuli
alitangaza kauli hiyo kufuatia ombi la wafanyikazi kupitia kwa katibu
mkuu bwana Nicholus Mgaya la kutaka wanusuriwe makali ya mfumuko wa bei
ya bidhaa muhimu.