Wednesday, 8 June 2016

Nyani azima umeme kote nchini Kenya

Nyani azima umeme kote nchini Kenya
Kampuni ya kuzalisha umeme nchini Kenya, KENGEN imetuma taarifa kwa vyombo vya habari ikiomba radhi kwa ukosefu wa umeme Kwa hapo jana.
Hilo sio jambo geni.
Mara kwa mara umeme hupotea nchini Kenya kwa sababu moja au nyengine, sawa tu na mataifa yote barani Afrika
Hata hivyo sababu walioitoa KENGEN kwa ukosefu huo wa umeme Kwa takriban saa nne kote nchini humo ndio imewaacha wengi wamepigwa na butwaa !
Nyani.
Maafisa wa polisi nchini Tanzania
Polisi nchini Tanzania wamepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia Jumanne wiki hii hadi hali ya usalama itakapotulia
Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari walinda usalama hao wamewataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi.
Taarifa hiyo imesema kuwa polisi hawatasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hilo.
Aidha maafisa hao wamewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi na badala yake kuwasihi waendelee kushirikiana katika kujenga Umoja wa taifa la Tanzania.
Polisi nchini Tanzania imeripoti kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya kisiasa vikitaka kufanya mikutano na maandamano .
Hata hivyo, maafisa hao kupitia vyanzo vyao mbalimbali vya habari wamebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.
 CHANZO: BBC

Aliyekuwa kocha wa Nigeria Stephen Keshi aaga dunia

Stephen Keshi
Mmoja wa wachezaji maarufu wa soka barani Afrika Stephen Keshi amefariki akiwa na umri wa miaka 54 ,shirikisho la Nigeria limethibitisha.
Nahodha huyo wa zamani wa kikosi cha Nigeria, Keshi,alikuwa mmoja wa watu wawili pekee kushinda michuano ya kombe la bara Afrika akiwa mchezaji na kocha.
Pia alifunza Togo na Mali,na aliwahi kuichezea timu ya Anderlecht ya Ubelgiji.Anadaiwa kuugua mshtuko wa moyo,kulingana na vyombo vya habari vya taifa hilo.

Tuesday, 31 May 2016

Hivi ndivyo alivyookolewa Alan Pulido

Image result for alan pulidoMamlaka nchini Mexico wameelezea namna mchezaji wa kimataifa Alan Pulido alivyookolewa baada ya kutekwa nyara mwishoni mwa juma.
Maofisa wanasema kuwa muda mchache baada ya kutekwa kwake Pulido alipambana na mmoja wa watekaji wake na kumyang'anya simu yake kisha akawapigia polisi.
Pulido, anayechezea klabu ya soka ya Olympiakos ya Ugiriki alijikata mkono wake wakati akijaribu kuvunja kioo kwenye mlango ili atoroke kabla ya polisi kuwasili katika eneo hilo.Alitekwa siku ya jumamosi na watu waliokuwa wamefunika nyuso zao wakati akitokea kwenye sherehe moja karibu na mji wake anaoishi wa Ciudad Victoria katika jimbo la Tamaulipas.

Samatta aiongoza timu yake kucheza Europa

Mbwana samatta
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameingoza KRC Genk kufuzu kucheza Ligi ya Europa baada ya kuichapa Sporting Charleroi kwa mabao 5­-1 na kushinda kwa jumla ya mabao 5-­3.
Kulingana na gazeti la Mwananchi, Samatta, ambaye katika mchezo wa kwanza walionyukwa 2-­0 alianzia benchi, jana aliaminiwa kuanza mchezo huo na kocha wake Peter Maes, akicheza pamoja na Nikos Karelis katika safu ya bora ya ushambuliaji.
Katika mchezo huo, Samatta alifunga bao moja na kutegeneza mengine mawili yaliyofungwa na Karelis ambaye alifunga magoli matatu katika mchezo huo, na Sandy Walsh akifunga bao moja kabla ya Sporting Charleroi kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na Jeremy Perbet.
Kulingana na Mwananchi,Genk, ikicheza kwenye uga wake wa nyumbani wa Cristal Arena ilianza mchezo kwa kasi na dakika 16, ilipata penalti baada ya Samatta kuangushwa kwenye eneo la hatari na kipa Nicolas Penneteau, ambaye alipewa kadi nyekundu

Monday, 30 May 2016

Kauli ya JPM kujitoa sadaka yazua mjadala


Kauli ya Rais John Magufuli kwamba yuko tayari kuutoa mwili wake sadaka katika kupambana na rushwa na ufisadi uku kuwasaidia wanyonge, imeibua mjadala huku wanasiasa wakitofautiana.

Akizungumza katika Mkutano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema: “Unapoona watu wanashangaashangaa sana (ni) kwa sababu hawakuzoea haya. Na walifikiri nitakuwa part of them (sehemu yao), never (haitatokea), not me (si mimi).
“Ni mara 10 nisiwe rais, nikachunge hata ndege, nikakae kijijini kuliko niwe Rais halafu nivumilie uozo huu unaofanyika. I’m saying never (nasema haitatokea).”
Rais Magufuli amekuwa akizitoa kauli kama hizo mara kwa mara, hasa anapowawajibisha baadhi ya watendaji wa Serikali, huku ikidaiwa kuna upinzani mkali ndani ya chama chake cha CCM, hali inayohisiwa kusababisha kauli hiyo.

Mkurugenzi wa Fordia, Bubelwa Kaiza alisema kauli hizo za Rais Magufuli zinaonyesha uzalendo wa kweli na amefanikiwa kufanya mambo yaliyowashinda marais waliomtangulia.
“Ndani ya CCM kuna upinzani mkali kutoka kwa makada. Kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita watendaji wa Serikali wamekuwa na mikakati ya kusaidia wezi na utapeli, hivyo anachofanya ni ‘revival strategy (mkakati wa kufufua),” alisema Kaiza.

Mpatanishi mkuu wa muungano wa upinzani nchini Syria amejiuzulu

Mpatanishi mkuu Syria
Mpatanishi mkuu wa muungano wa upinzani nchini Syria amejiuzulu katika kile anachosema kuwa, kuvunjika kwa mazungumzo ya amani, yenye nia ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka mitano sasa.
Mohammad Alloush, anayetoka kwenye kamati kuu ya upatanishi HNC, amesema kuwa anajiondoa kwa sababu mazungumzo hayo yanayoungwa mkono na Umoja wa mataifa huko Geneva, hayajazaa matunda au kutanzua matatizo wanayopitia raia wa Syria waliozingirwa na vita.
Kamati kuu ya mazungumzo hayo ya amani iliahirisha shughuli zake mwezi Aprili na hakuna tarehe ambayo imewekwa ya kurejelewa kwa mazungumzo.