Friday, 4 July 2014

Wanamgambo wa kundi la Hamas wasitisha mapigano

Wapiganaji wa kundi la Hamas
Taarifa kutoka Gaza zinasema wapiganaji wa Palestina wa Hamas kimesema kipo tayari kusimamisha mapigano ya maroketi kwenye miji nchini Israel na kutaka kuhakikishiwa kuhusu mashambulio ya anga katika ukanda wa Gaza nayo yasitishwe mara moja.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yalikuwa yakisimamiwa na maafisa kutoka nchini Misri.
Israel imesema itapeleka vikosi zaidi vya majeshi yake katika mpaka wa ukanda wa Gaza, ili kujibu mashambulio ya maroketi yaliyofanywa na Palestina, ndani ya ardhi ya Nchi yake.
Katika maeneo ya mashariki mwa Jerusalem kumeshuhudiwa siku ya pili ya maandamano ya kupinga mauwaji ya kijana wa kipalestina. Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika hatimaye hii leo Ijumaa.
Hata hivyo maafisa wakuu wa Majeshi ya Israel wamesema hatua hiyo ni ya kujilinda na wala haina nia ya kuchochea machafuko zaidi kati yake na Palestina.

Mugabe awatimua wakulima wazungu Zimbabwe

Wakosoaji wa Mugabe wanasema sera ya mageuzi ya mashamba ilimalizika miaka miwili iliyopita
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wakulima wazungu waliosalia nchini humo kuondoka na kuwaachia mashamba wazalendo wa nchi hiyo.
"hatuwataki wakulima wazungu, kumiliki mashamba yetu, lazima waondoke,'' Mugabe aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara.
Chama cha wakulima wazungu, kimesema kuwa matamshi ya Mugabe yanasikitisha sana na kwamba taharuki ya kibaguzi imeanza kutanda.
Wakosoaji wa Rais Mugabe, wanasema kuwa sera yake kutaka kumiliki mashamba yote yanayomilikiwa na wazungu, ndio ilisababisha kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 200-2009
Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 90, ametawala Zimbabwe tangu nchi hiyo kujipatia uhuru mwaka 1980.
Alichaguliwa tena mwaka jana kwa asilimia 61 ya kura, na kumshinda mpinzani wake wa jadi Morgan Tsvangirai.
Chama cha Mugabe pia kilishinda viti vingi vya bunge na kupata 160 kati ya viti 210.
Mdadisi wa kisiasa nchini humo Stanley Kwenda anasema kuwa matamshi ya Mugabe, yanashangaza sana kwani serikali ilimaliza mageuzi ya sera ya umiliki wa mashamba miaka miwili iliyopita.
Inaonekana kwamba Mugabe anataka kuhujumu hali mbaya ua kiuchumi nchini humo kwa kuzungumzia maswala mengine ambayo hayana umuhimu kwa sasa.
Wananchi wa Zimbabwe wanakumbwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na kufungwa kwa makampuni .
'Wasiwasi'
Mkulima huyu mzungu Zimbabwe,anatizama uharibifu uliofanyiwa nyumba yake baada ya watu kuivamia
"usiwe mkarimu sana kwa wakulima wazungu. Mashamba ni yako sio yao,'' alisema Mugabe alipotembelea mkoa wa Mashonaland , Magharibi mwa nchi.
Mtamshi ya Rais Mugabe, yalisababisha wasiwasi miongoni mwa wakulima wazungu. Hii ni kwa mujibu wa mkuu wa muungano wa wakulima wazungu Hendricks Olivier.
Ni wakulima 100 hadi 150 wazungu waliosalia nchini Zimbabwe, alisema Hendricks.
Maelfu ya wakulima walilazimika kuyaacha mashamba yao na kurejea walikotoka baada ya serikali kufanya mageuzi ya sera ya umiliki wa ardhi miaka 15 iliyopita.

Wednesday, 2 July 2014

Costa mchezaji rasmi wa chelsea sasa

Chelsea imeafikiana na Atletico Madrid kumnunua Costa
Chelsea imedhibitisha kuwa imekubaliana na mshambulizi wa Atletico Madrid na Uhispania Diego Costa sasa atashuka Stamford bridge msimu ujao.
Klabu hiyo ya London imedhibitisha kuwa imeafikiana na Atletico Madrid kutumia kipengee cha kumnunua mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 25 .
Hadi kufikia sasa haijadhibitisha gharama yake itakuwa kiasi gani lakini wandani katika klabu hiyo wanasema Costa huenda akaigharimu The Blues takriban dola milioni 55m
Chelsea imeafikiana na Atletico Madrid kumnunua Costa
Mzaliwa huyo wa Brazil aliifungia Atletico mabao 35 msimu uliopita na kuisadia timu hiyo kufuzu kwa fainali ya kombe la mabingwa barani ulaya walikoshindwa na mahasimu wao wa jadi Real Madrid .
Kocha wa wa the Blues Jose mourinho amekuwa akiimarisha kikosi chake kwa kusajili nguvu mpya na pia kuna dukuduku kuwa wachezaji wazoefu wa Chelsea Ashley Cole na Frank Lampard huenda wakaondoka Stamford Bridge.
Mwezi uliopita Mourinho alimsajili aliyekuwa kiungo wa Arsenal Cesc Fabregas huku kandarasi ya kipa Mark Schwarzer ikiongezwa muda .

Taifa stars ya chapwa 4 2 na Botswana

taifa-stars-2014Timu ya Taifa (Taifa Stars) imevurumishwa mabao 4-2 katika mechi ya kirafiki na Botswana jana.
Mechi hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Gaborone ni sehemu ya maandalizi ya Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabao ya Taifa Stars yalifungwa na Khamis Mcha `Vialli` na nahodha wa Azam fc, John Raphael Bocco `Adebayor`
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kurejea nchini Julai 6 mwaka huu kuendelea na programu nyingine kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.
taifa-stars-2014
Timu ya Taifa (Taifa Stars) imevurumishwa mabao 4-2 katika mechi ya kirafiki na Botswana jana.
Mechi hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Gaborone ni sehemu ya maandalizi ya Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao ya Taifa Stars yalifungwa na Khamis Mcha `Vialli` na nahodha wa Azam fc, John Raphael Bocco `Adebayor`
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kurejea nchini Julai 6 mwaka huu kuendelea na programu nyingine kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2955#sthash.epmHA7HY.dpuf

13 wafariki katika mapigano mpakani huko Uganda

Watu 13 wafariki katika mapigano mpakani 

Watu 13 wamefariki dunia katika mapigano baina ya wanajeshi wa Uganda na wanachama wa Seleka.

Imearifiwa kua katika Mapigano yaliyozuka mpakani mwa Jamhurin ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati baina ya wanachama wa Seleka na wanamgambo wa jeshi la Uganda watu 13 walipoteza maisha.
Katika maelezo yake msemaji wa jeshi la Seleka, Goma Narkoyo alisema “siku iliyopita, palitokea mapigano baina ya askari wa Uganda na askari wa Seleka kutokana na kutoelewana na kusababisha askari 1 na wanachama 2 wa Seleka kufariki.
“Kiongozi wa jeshi la UpinzanI, Joseph Kony anatafutwa kwa visingizio vya ulinzi kwa ajili ya Uganda, Narkoy alisema “ kwa miaka 6 sasa wanamsaka Kony hata hivyo hawajapata chochote. Wao wanafanya biashara za dhahabu, pembe za ndovu na mbao. Wameshindwa kusimamia majukumu yao, nasi tunataka waondoke”.
Msemaji wa jeshi la Uganda, Yarbay paddy Ankunda alisema mwanajeshi mmoja aliwaua wanachama 11 wa Selek ana kuchukua silaha walizokuwa nazo.
Kumekua na ugomvi wa muda mrefu baina ya Jeshi la upinzani la Bwana na Uganda.

Wanne wafariki dunia kwa ajali ya ndege kenya

4 wafariki katika Ajali ya ndege KenyaWafanyakazi 4 wa shirika moja la ndege ya kubebea mizigo nchin kenya wameaga dunia baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kugonga jengo la orofa 2.

Ndege hiyo ya kubebea mizigo ilikumbwa na ajali hiyo punde tu baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta. Inasemekana kuwa huenda ndege hiyo iligonga nguzo ya umeme kabla ya kugonga jengo lile. Uchunguzi wa kubaini chanzo cha ajali hiyo umeanzishwa.

Tohara yasababisha vifo ya wavulana 19 Afrika kusini

Wizara ya Afya nchini Afrika Kusini inasema kuwa wavulana kumi na tisa wameaga dunia mwaka huu katika sherehe za kitamaduni za kuwapasha tohara wavulana.
Tohara hiyo ni utamaduni unaopewa heshima kubwa katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo.
Utamaduni wa tohara ni muhimu kwa vijana hasa kwa kuwa ni njia ya vijana kuingia utu uzima, lakini baadhi hufariki wakipitia utamaduni huo na wengine hupoteza sehemu zao nyeti.
Vijana 19 wamefariki kufika sasa na wengine 50 wako hospitalini.
Wanapokea matibabu ya kukosa maji mwilini, sehemu zao za siri kuoza na majerahe mengine mabaya.
Wazee wa kijamii wasiokuwa na mafunzo ya kufanya tohara ambao huendesha vituo vya kuwapasha tohara vijana wamelaumiwa kwa vifo kama hivyo.
Katika baadhi ya visa ambavyo vimeripotiwa, vijana hutoroka na kujiunga na vijana wengine wanaokwenda katika vituo hivyo haramu bila ya idhini ya wazazi.
Serikali imewasihi wazee wa kijamii kushirikiana na watu wenye uwezo wa kitaalamu na madaktari ili kuwapasha tohara vijana na kuzuia vifo.
Mwezi jana watu 23 walikamatwa kwa vifo vya vijana waliofariki kutokana na athari za kupashwa toihara.