Raia wa Burundi wamekuwa wakitoroka mitaa mingi ya mji wa Bujumbura
Ubelgiji
imewashauri raia wake kuondoka Burundi, huku Muungano wa Ulaya nao
ukipunguza maafisa wake wanaohudumu huko kutokana na kuongezeka kwa
machafuko.
Balozi wa EU nchini humo Patrick Spirlet amesema hatari ya kutokea mapigano zaidi imeongezeka.
Hayo
yamejiri huku idara ya Amani ya Usalama ya Muungano wa Afrika
ikikutana mjini Addis Ababa kujadili mpango wa kutuma walinda amani
nchini humo.
Ufaransa
imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya
120 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.
Watu 120 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.
Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.
Watu
wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo
wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na
Ujerumani ilikuwa ikiendelea.
Rais wa Nigeria
Muhammadu Buhari hatimaye ametangaza wizara na mawaziri
watakaozisimamia, miezi saba baada yake kushinda uchaguzi wa urais.
Nafasi
muhimu ya waziri wa fedha ameikabidhi mwanauchumi Kemi Adeosun,
aliyesomea Uingereza kabla ya kurejea Nigeria na kuhudumu kama kamishna
ya fedha jimbo la Ogun.
Jenerali mstaafu Mansur Dan Ali atakuwa
Waziri wa Ulinzi, na kazi yake kuu itakuwa kuongoza vita dhidi ya
wanamgambo wa Boko Haram.
Gavana wa zamani wa jimbo la Lagos
Babatunde Fashola ameteuliwa waziri wa kawi, ujenzi na makazi na
anakabiliwa na kibarua cha kutatua mzozo wa umeme Nigeria.
Mwanasiasa mkongwe ambaye pia ni mkulima Audu Ogbe ameteuliwa waziri wa kilimo.
Nigeria
ina ardhi kubwa ambayo ikutumiwa vyema inaweza kubuni nafasi za kazi na
kupunguza utegemezi wa mafuta, wadadisi wanasema.
Kuzinduliwa kwa baraza hilo lenye mawaziri 36 kumefanyika miezi saba baada ya uchaguzi wa urais.
Buhari alishinda uchaguzi uliofanyika Machi
Bw Buhari aliyechaguliwa Machi alikuwa ameahidi
kukabiliana na ufisadi na ukosefu wa usalama, na aliahidi kuteua watu
wenye ujuzi na wasio na ila.
Mhariri wa BBC Hausa Mansur Liman
anasema baraza hilo la Rais Buhari litashangaza watu na hasa uteuzi wa
Bi Adeosun kuwa waziri wa fedha. Wengi walitarajia Okechukwu Enelemah,
aliyeteuliwa waziri wa biashara na uwekezaji, angeteuliwa waziri wa
fedha.
Rais Buhari pia ameshangaza wengi kwa kumteua mkuu wa
zamani wa jeshi Jenerali Abdurrahman Dambazau kuwa waziri wa mambo ya
ndani. Wengi walitarajia angeteuliwa waziri wa ulinzi.
Amina
Mohammed, mshauri wa zamani wa mkuu UN Ban Ki-Moon kuhusu maendeleo
endelevu, alitarajiwa kuteuliwa waziri wa mipango lakini ameteuliwa
waziri wa mazingira.
Klabu ya mchezaji huyo ilishindwa kwenye mechi hiyo
Mchezaji wa Oakland
Raiders Ray-Ray Armstrong anachunguzwa na maafisa wa polisi kwa tuhuma
za ‘kubweka’ na kujipiga kifua mbele ya mbwa wa polisi.
Armstrong, 24, anadaiwa kuinua shati lake na kumchokoza mbwa huyo kabla ya mechi ya NFL dhidi ya Pittsburgh Steelers Jumapili.
Akipatikana
na hatia, huenda akashtakiwa na kosa la kumchokoza mbwa wa polisi,
ambalo ni kosa la ngazi ya tatu jimbo la Pennsylvania.
Rais wa Equatorial
Guinea Teodoro Obiang Nguema, ambaye ameongoza taifa hilo kwa miaka 36,
amesema atawania tena, shirika la habari la AFP limeripoti.
Kiongozi
huyo mwenye umri wa miaka 73 alisema kupitia kituo cha redio cha taifa
kwamba ameungwa mkono na chama chake kuwania urais kwa muhula mwingine
wa miaka saba mwaka ujao.
Chama cha Obiang cha Democratic Party of
Equatorial Guinea kilishinda viti 99 kati ya 100 vya ubunge katika
uchaguzi mkuu wa 2008.
Alishinda uchaguzi wa urais mwaka mmoja baadaye kwa kupata 95% ya kura.
Obiang ni mmoja wa viongozi
waliokaa madarakani muda mrefu zaidi Afrika.
Mamia
ya wanachama wa chama cha mapinduzi CCM katika wilaya ya Kibondo
wameanadamana na kuvamia ofisi za chama hicho wakipinga mgombea
aliyeshinda katika kura za maoni Jamal Abdalah kutoteuliwa na
halmashauri kuu ya taifa ya CCM kuwania ubunge katika jimbo la Muhambwe
wilayani Kibondo.
Mamia
ya wanachama wa chama cha mapinduzi CCM katika wilaya ya Kibondo
wameanadamana na kuvamia ofisi za chama hicho wakipinga mgombea
aliyeshinda katika kura za maoni Jamal Abdalah kutoteuliwa na
halmashauri kuu ya taifa ya CCM kuwania ubunge katika jimbo la Muhambwe
wilayani Kibondo.