Thursday, 31 March 2016

Mahakama yatupilia mbali kesi Uganda


Mahakama ya juu zaidi nchini Uganda imefutilia mbali kesi iliyokuwa ikipinga ushindi wa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi uliopita.
Mahakama hiyo ilisema kuwa licha ya kuwepo kwa dosari nyingi za uchaguzi, matokeo ya mwisho hayakuathiriwa.

Kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi wametangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.

Rais wa Tanzania John Magufuli.
 Kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi wametangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.
Hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya marekani kuondoa msaada wa dola 472 wa kufadhili miradi ya maendeleo kutokana na jinsi uchaguzi wa kisiwa cha Zanzibar ulivyoendeshwa.
Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya.

Tuesday, 29 March 2016

Wanariadha wala sabuni kwa kuwa hawajui kingereza

Sabuni
Wanariadha waliokuwa wanakimbia mbio ndefu za marathon walijipata wamekula sabuni baada ya kudhania kwamba zilikuwa chakula kutokana na kukosa kuelewa lugha ya kiingereza.
Takriban wanariadha 20,000 katika mbio za Qinyuan marathon kusini mwa mkoa wa Guangdong nchini Uchina walipata zawadi mda mfupi baada ya kumaliza mbo hizo katika utepe kulingana na gazeti la kila siku nchini humo la Peoples daily.
Wakidhania kwamba walikuwa wanakula chakula,wanariadha hao badala yake walikuwa sabuni zilokuwa zikinuka harufu nzuri .

Wamexico washerehekea sikukuu ya pasaka kwa kuchoma sanamu a Donald Trump

Wa-Mexico wachoma mfano wa 'Trump'
Raia wa Mexico wanaosherehea sikukuu ya pasaka wamekuwa wakichoma sanamu za mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Republicans Donald Trump.
Mojawapo ya tukio hilo la kushangaza limefanyika katika kitongoji kimoja cha wakaazi walio na kipato cha chini kiitwacho La Merced.
Wakaazi wengi wa La Merced wamejitokeza kushuhudia kuchomwa kwa kikaragosi cha Trump badala ya kile cha yule mfuasi wa Yesu Kristu aliyemsalito Judas Iscariot.

Tanzania yasikitika kunyimwa pesa za MCC

Tanzania imehuzunishwa na hatua ya bodi ya shirika la changamoto za milenia (MCC) kusitisha msaada
wake wa awamu ya pili wa dola milioni 472.8 ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja pesa za Tanzania.
Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga ameelezea kushtushwa kwake na hatua hiyo ya bodi ya MCC akisema "imepuuza hatua kubwa tu zilizopigwa kidemokrasia" nchini humo.
''Inasikitisha kuwa demokrasia yetu inatathminiwa tu na matokeo ya uchaguzi wa visiwani Zanzibar,''
Waziri wa mambo ya nje bwana Augustine Mahiga
Kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar Bw Mahiga anasema kuwa Tanzania, ilifanya kila kitu kuambatana na sheria na katiba ya nchi wala hakuna tatizo ama ukiukwaji wa sheria.
Mahiga anasema kuwa huo ni uamuzi wao na kwa sababu hela hizo ni zao wanauhuru wa kuzitumia watakavyo ila anahoji kwanini uamuzi huo uliafikia bila ya majadiliano na serikali ya muungano ya Tanzania.

Monday, 21 March 2016

Tetesi za Usajili barani Ulaya

Kocha wa zamani wa Leicester Nigel Pearson amepewa kipaumbele kuja kuchukua mikoba ya kocha wa Aston Villa Mfaransa Remi Garde anayetegemewa kutimuliwa siku za hivi karibuni. (Chanzo Daily Mail)
Shirikisho la soka nchini Uingereza (FA) linataka kujaribu kwa mara ya mwisho kumzuia mshambuliaji wa Arsenal Alex Iwobi, 19, kuchukua uraia wa Nigeria. (Chanzo Daily Mirror)
Mabingwa wa nchini Italia Juventus watajaribu kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud, 29, mwishoni mwa msimu ikiwa watamkosa chaguo lao namba moja, Edison Cavani, 29, wa Paris St-Germain. (Chanzo Tuttosport kupitia Daily Express)

Watu wawili Mkoan Dar Es Salaam wamefariki dunia kwa maradhi ambayo dalili zake zinafanana na ugonjwa wa ebola.



Watu wawili wamefariki dunia kwa maradhi ambayo dalili zake zinafanana na ugonjwa wa ebola.






Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi wa Magonjwa MNH, Dk Praxeda Ogweyo alisema wamewapokea wagonjwa hao wawili,  lakini vipimo havijaonyesha kama wana ebola.  “Ni kweli kuwa tumewapokea wagonjwa hao wawili na vipimo vya mgonjwa wa kwanza kinaonyesha hana ebola, lakini bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina kujua ni ugonjwa gani,” alisema.