Monday 1 September 2014

Kocha wa simba ampa Maximo Ushauri



juma kaseja 
MARCIO Maximo amefunga mjadala kwa kutamka kwamba Deo Munishi ndiye kipa namba moja wa Yanga, lakini kocha wa makipa wa Simba, Idd Pazi amesema kuwa kati ya makipa wote Tanzania anayestahili kuwa namba moja ni Juma Kaseja.
Pazi alisema kuwa katika nafasi hizo kunakuwa na makipa wa aina mbili, kipa mwenye kipaji na kipa wa mazoezi huku akimtaja Kaseja kuwa ni kipa mwenye kipaji.
Alisema kuwa mbali na kuwa na kipaji, lakini Kaseja ni kipa anayejituma bila kukata tamaa japo amekuwa akipewa tuhuma mbalimbali kutoka kwa mashabiki.
“Sijawahi kuona kipa mzuri kama Kaseja, kwanza ana kipaji, anajitambua na hata ukikutana naye mara nyingi mazungumzo yake ni soka na maendeleo yake katika hilo, ni kipa ambaye yupo wazi kutaka kujua jambo litakalomsaidia,” alisema.
“Makipa Tanzania wapo wengi, lakini wengi wao ni makipa wa mazoezi kwamba afanye sana mazoezi ndipo alinde kipaji chake.
“Lakini hiyo ni tofauti kabisa kwa Kaseja, nimemfundisha na hata sasa hivi huwa anahitaji kufundishwa pale anapokuwa na muda wa ziada, hivyo unaona kabisa kwamba huyu ni kipa mwenye malengo.
“Ndiyo maana ninasema Kaseja ndiye namba moja nchini.”
Alisema kuwa wengi wanadai umri wa Kaseja umekuwa mkubwa ndiyo maana kiwango chake kimeshuka, lakini yeye alisistiza kuwa kipa huyo ana miaka zaidi ya miwili katika soka.
“Hapa Simba kuna huyu kijana Manyika Peter, kama hatalewa sifa na akajitambua naye atafika mbali kama Kaseja,” alisema Pazi.

No comments: