Monday 1 September 2014

Kwezera ashangaa wing wa mashabiki wa simba



KIUNGO wa Simba, Mrundi Pierre Kwizera amesema hajawahi kucheza timu yenye wingi wa mashabiki kama klabu hiyo ya Msimbazi na ndiyo wanamshawishi ajitume na kufanya kazi kwa bidii ili kuwapa kile wanachokitaka.
Kwizera amesajiliwa na Simba msimu huu, akitokea nchini Ivory Coast alikokuwa anakipiga klabu ya Afad Abdijan.
Ameliambia ukomboz akisema: “Sijawahi kucheza kwenye klabu yenye mashabiki wanaopenda timu yao kama Simba, nimependa sana.
“Mashabiki hawa wananipa raha na ndiyo wanaonishawishi nifanye kazi yangu kwa ustadi na nguvu ili niwaridhishe kwa kuwapa kile kitu wanachopenda.”
Kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Burundi anayevaa jezi namba nane, amekuwa akifanya vizuri kwenye mechi za kirafiki alizocheza pamoja na mazoezini na kuwashawishi mashabiki wamkubali.
Beki wa kikosi hicho cha Msimbazi, Nassor Masoud ‘Chollo’ ametamka kuwa mchezaji atakayeshindwa kuishi na kufanya kazi na kocha wao mkuu wa sasa, Mzambia Patrick Phiri atakuwa na matatizo makubwa.
Chollo anafanya kazi na Phiri kwa mara nyingine baada ya kumfundisha hapo awali na kumwelezea, huwa hana matatizo na mchezaji yeyote kama utamsikiliza na kumfuata anachokitaka.
Chollo aliambia ukombozi “Makocha wengine huwa na matatizo lakini kwa huyu Phiri utakuwa unamwonea, tena kwa mchezaji yeyote anayeshindwa kufanya naye kazi, atakuwa na matatizo binafsi.”
“Nimekaa na makocha wengi, lakini kwa huyu jamaa ni sawa na mzazi kwa kila mchezaji, anakuelekeza na unapokosea anakaa na wewe kama mzazi mnayaweka sawa, hadi mtofautiane, lazima mchezaji husika atakuwa na matatizo.”

No comments: