Monday 25 August 2014

Mchezaji afa uwanjan baada ya kutupiwa kitu na washabik

Mchezaji kutoka Cameroon Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kurushiwa kitu na mashabiki katika mchezo wa ligi nchini Algeria. Ebosse, 24, alithibitishwa kuwa amefariki baada ya kufikishwa hospitali katika eneo la Tizi Ouzou, mashariki mwa mji mkuu, Algiers. Mshambuliaji huyo wa klabu ya JS Kabylie, ambaye alikuwa amefunga goli moja katika mchezo huo waliopoteza kwa 2-1, dhidi ya USM Alger aligongwa na kitu hicho baada ya mpira kumalizika, wakati wachezaji wakiwa wanatoka uwanjani. Wizara ya mambo ya ndani ya nchi imetaka uchunguzi kufanyika mara moja. Haijathibitishwa ni kitu gani hasa alichogongwa nacho, lakini gazeti moja la Algeria limesema mashabiki walikuwa wamekasirishwa na kufungwa na walikuwa wakirusha mawe. Taarifa iliyotolewa na klabu yake imesema :”alikufa kutokana na jeraha la kichwani” baada ya kurushiwa kitu mwisho wa mchezo. Rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika, Issa Hayatou ametoa taarifa inayolaani tukio hilo

No comments: