Wednesday, 6 August 2014

Picha za mwanamitindo wa India zazua balaa Nchini Humo

Picha za wanamitindo zilizopigwa kwenye basi zikionyesha mwanamke akionekana kama anayebakwa na wanaume, zimezua hisia kali kwenye mitandao ya kijamii nchini India.
Watu wengi wamesema kuwa picha hizo zinaonekena kusifu kitendo cha ubakaji kilichomkuta mwanafunzi mmoja mjini Delhi kwenye basi mwaka 2012.
Mwanafunzi huyo ambaye aliga baadaye, alibakwa na genge la wanaume.
Picha za mpiga picha Raj Shetye ambaye alipiga picha hizo, zinaonyesha mwanamke akioenekana kupigania maisha yake akiwa amezuiliwa na wanaume wawili kwenye kiti cha basi.
Ni kitendo ambacho kinaleta hisia kali kwa watu wengi na kumbukumbu za unyama uliotendewa msichana wa shule kwenye basi hadi akafa.
Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wanasema picha hizo ni za kukera na zinatisha .
Bwana Shetye hata hivyo amejitetea akisema picha hizo ni za kuonyesha tu hali inayowakumba wanawawake wengi nchini huo wala sio kuonyesha ubakaji.
Hata hivyo picha hizo ziliondolewa kwenye mtandao huo wa Behance baada ya hisia kali kutoka kwa watumiaji waTwitter na Facebook.
Ubakaji wa msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 23 ulisababisha maandamano makubwa nchini humo na hata kulazimisha maafisa wakuu kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na ubakaji
shirika la utangazaji la Uingereza BBC lilijaribu kumtafuta Bwana Shetye aweze kujieleza kuhusu picha hizo ingawa hatukufanikiwa badli vyombo vya habari vilimnukuu akisema hakua na nia ya kuleta kumbukumbu mbaya kuhusu kitendo cha ubakaji kilichozua hasira kote nchini India.

No comments: