Jumapili Simba walifanya Mkutano Mkuu wa wanachama ambapo walifanya mabadiliko ya Katiba katika baadhi ya vipengele huku Ibara ya 25 kipengele cha 8(iii) kimeonekana kumrudisha kundini kihalali Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.
Kigogo huyo amekuwa tishio kwa Yanga haswa kutokana na ushawishi wake.
Kabla ya mabadiliko hayo, kipengele hicho ambacho
kinahusu viongozi watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa uchaguzi ni
wajumbe watano wa Kamati ya Utendaji, pia Rais atateua wajumbe wengine
watano wa Kamati ya Utendaji ambao anaweza kuwabadilisha kwa kadiri
anavyoona inafaa.
Kipengele hicho kimeendelea kuelezea kuwa wajumbe
hao wa kuteuliwa wanatakiwa kuwa na sifa zile zile wanazotakiwa kuwa
nazo wajumbe wa kuchaguliwa na wanachama.
Hivyo katika marekebisho ya kipengele hicho ni
kwamba wajumbe watano wa Kamati ya Utendaji watachaguliwa na wanachama,
lakini Rais atateua wengine watano wa kamati hiyo ambao anaweza
kuwabadilisha kwa kadiri anavyoona inafaa na hawatakiwi kuwa na sifa
kama zile za wajumbe wa kuchaguliwa.
Hiyo inamaana kwamba wajumbe hao wa kuteuliwa
wanatakiwa kuwa na sifa ya uanachama wa klabu hiyo tu. Tayari Rais wa
klabu hiyo, Evans Aveva ameteuwa wajumbe watatu ambao ni Mohamed
Nassoro, Salim Abdallah na Musley Saleh hivyo amebakiwa na nafasi mbili
za kujaza.
Kwa mamlaka aliyona sasa, Aveva anaweza kutumia
nafasi hiyo kumpachika Hans Poppe ambaye hawezi kugombea nafasi yoyote
ndani ya Simba kutokana na kubanwa na Ibara ya 26 (4) kinachosema
mgombea asiwe aliyewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai kwa kuhukumiwa
kifungo.
Tayari Hans Poppe ambaye ni mmoja wa wanachama wa
Simba wenye ushawishi mkubwa alishatamka wazi kuwa hawezi kugombea tena
Simba kutokana na kubanwa na kipengele hicho
No comments:
Post a Comment