Wednesday, 6 August 2014

Mbeya City kujenga kiwanja cha Kisasa

UJENZI wa Uwanja wa kisasa wa Mbeya City utaanza mwishoni mwa Agosti hii ambapo wataanza kujenga viwanja viwili, kimoja cha mazoezi na kingine cha mechi.
Eneo la uwanja huo utakaoitwa Mbeya City Arena upo lipo Iwambi jijini Mbeya ambapo ni nje kidogo ya jiji hilo na una ukubwa wa hekta mita 5.7.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, ameliambia Mwanaspoti akisema: “Mwisho mwa mwezi huu ni lazima tuanze kujenga kwani tayari wananchi wamevuna mazao yao, pia tunasubiri ramani ya uwanja ambayo tumeipa kazi kampuni moja hapa jijini, tanaanza na uwanja wa mazoezi mambo mengine yatafuata hapo baadaye.”
Kuhusu maandalizi ya timu, Kimbe alisema kuwa wamewasilisha majina ya wachezaji wao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo wataingia kambini Agosti 15 akiwamo Saady Kipanga ambaye inasemekana tayari yupo jijini Mbeya.
Kipanga alikuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao walidaiwa kusajiliwa na Simba msimu ujao, lakini dili hilo liliingia mchanga baada ya wajumbe wa Kamati ya Usajili kutokubaliana na usajili wake na hivyo kumsajili Elius Maguli wa Ruvu Shooting.

No comments: