Said Kipanga |
Awali viongozi wa Kamati ya Usajili kwa
ushirikiano na viongozi wengine wa Simba, walikubaliana kufuta usajili
wa mchezaji huyo. Lakini baadaye mmoja wa vigogo hao (jina tunalo)
aliliibua suala hilo upya juzi Jumatano kwa madai kuwa tayari
amemsainisha Kipanga mkataba wa miaka miwili.
Siku hiyo kamati hiyo ilikutana kujadili
mustakabali mzima wa usajili na kufunga kazi hiyo ili kocha apate muda
wa kukaa na wachezaji husika, lakini ishu ya Kipanga ikatibua uelekeo wa
kikao. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zacharia
Hans Poppe.
Suala hilo lilionekana kuwagawa baadhi ya wajumbe
wa kamati ambapo walio wengi walionekana kupinga juu ya usajili huo huku
wajumbe watatu pekee wenye ushawishi wa kifedha wakiunga mkono. Wajumbe
wengi walikuwa wakimtaka Elius Maguli ambaye yupo kwenye orodha ya
matakwa ya kocha.
Mbeya City watoa tamko
Uongozi wa Mbeya City umesema kuwa ulipokea barua
ya kiongozi mmoja wa juu wa Simba juu ya maombi ya usajili wa Kipanga,
Deus Kaseke na Anthony Matogolo na kuwapa masharti ya kutimiza.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Emmanuel Kimbe, alisema
baada ya kuijibu barua hiyo ya Simba, hawakupokea mwendelezo wowote wa
mawasiliano juu ya usajili hivyo wanashangaa kusikia Kipanga kasajiliwa
Simba wakati bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu na klabu hiyo na
kama ni kweli watashtaki.
“Kuna barua ilitumwa kutoka Simba na tuliwajibu,
lakini hakuna majibu yaliyorudi kutoka kwao, hivyo tunasubiri itakuwaje
maana tunasikia tu kuwa wamemsajili, huo utakuwa usajili wa kinyemela na
uvunjaji wa kanuni za usajili, sisi tumewasiliana na TFF juu ya hilo.
“Kanuni zipo wazi huwezi kufanya mazungumzo na
mchezaji ambaye ana mkataba kuanzia mwaka mmoja na klabu nyingine labda
angebakiza miezi sita, wachezaji wetu wanatakiwa kufika kambini, Kipanga
ni mmoja wao,” alisema Kimbe.
Kuhusiana na usajili wa Maguli ndani ya Simba, ukombozi inajua kwamba Wekundu wa Msimbazi hao wameshatuma ofa JKT
Ruvu. Jana Alhamisi walitarajia kumalizana naye huku uongozi wake
ukikiri kupokea barua kutoka Simba.
“Tunakutana viongozi kujadili, lakini hatuwezi
kumzuia mchezaji ambaye ameonyesha nia ya kwenda kucheza timu yoyote
kwani tukimzuia hatafanya vizuri kwetu, Simba wametuma barua lakini
haina ofa yoyote ila tutamruhusu akachezea Simba kwani ndio timu
aliyoipenda, naamini tutakubaliana na hatuwezi kuwakomoa kwa kutaka
fedha nyingi,” alisema Msemaji wa JKT Ruvu, Masau Bwire.
No comments:
Post a Comment