Sunday, 15 December 2013

UGOMVI WA KIMAPNZ WASABABISHA MUME KUUA MTOTO WA KAMBO HUKO IRINGA

Mwenyekiti wa mtaa wa pangani kata ya Makorongoni mjini Iringa Salum Kibaya akiutazama mwili wa mtoto Raymond Ben Mangungu (2) aliyeuwawa kwa kukabwa shingo na baba wa kambo wakati wa ugomvi wa kimapnzi kati ya mwanaume huyo na mama wa mtoto huyo usiku wa leo.
Askari polisi akitazama mwili wa mtoto huyo.
Hali ilivyokutwa ndani ya chumba hicho baada ya tukio.
Wananchi wa Makorongini wakimtazama mwanamke huyo wakati akihojiwa na kaka wa mtuhumiwa wa mauwaji hayo.
Mama wa mtoto Raymond katikati akimsimulia shemeji yake jinsi ambavyo mpnzi wake alivyoua mtoto ,kushoto ni mama mzazi wa mwanamke huyo.Huyu ndie mzazi wa mtoto aliyeuwawa Bi Kudra Kahemela (23)Wanawake wa mtaa wa Pangani Iringa wakiuhifadhi mwili wa mtoto Raymond leo.
KATIKA hali isiyo ya kawaida mwanaume mmoja mkazi wa mtaa wa Pangani kata ya Makorongoni katika Manispaa ya Iringa Hamis Said maarufu kwa jina la Mwarabu amemuua kinyama mtoto Raymond Ben Mangungu (2) kutoka na ugomvi wa kimapnzi kati yake na mama wa mtoto huyo ambae kwake ni mpnzi wake .
Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo wa mauwaji ya mtoto huyo alikuwa amelewa pombe kupita kiasi na si mara ya kwanza kulewa kiasi hicho na kutishia kufanya mauwaji dhidi ya mtoto huyo wa kambo kwa kile alichokuwa akidai kuwa ni fedhea kwake kuishi na mwanamke ambae ana watoto wawili ambao si damu yake.
Wakizungumzia juu ya tukio hilo mashuhuda wa tukio hilo kwa sharti la kutotaja majina yao walisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa Mwarabu kumpiga mwanamke huyo na familia yake kwa madai kuwa hataki kuwaona watoto hao wakiendelea kuishi katika nyumba hiyo ambayo ameipanga yeye .
" Huyu bwana Mwarabu alikuwa akifanya kazi ya kuuza korosho mitaani na akirudi usiku amekuwa mkali kwa mwanamke huyo ambae alikuwa akidai kuwa bado amekuwa na mahusiano na baba wa watoto hao wawili .....hata hivyo sisi kama majirani tumekuwa tukishindwa kuwaamua kutokana na mwanaume kuwa na tabia ya kulewa pombe kupita kiasi na hata tukio hili tulijua ni kawaida yao "
Mtoto Tinito Mangungu (6) ambae ni kaka na marehemu alisema kuwa baba yao huyo mdogo alifika usiku na kuwataka wote kuamka kitandani na kuwa hakuna mtu atakayelala katika chumba hicho kama si damu yake.
"Baba mdogo (Mwarabu) alirudi usiku akiwa amelewa na kusema hakuna mtu kulala kitandani na kuanza kumpiga mama kwa meza na viti huku sisi tukilia kumtaka asimpige mama yetu....baada ya hapo alimchukua mdogo wangu na kuanza kumkaba shingo na kumwacha kitandani akiwa amelama bila kuamka hadi sasa mama anasema amekufa"
Akielezea juu ya mkasa huo uliosababisha mauwaji ya mtoto Raymond mama mzazi wa mtoto huyo Bi Kudra Kahemela (23) alisema kuwa kwa upande wake baada ya kutishiwa kuuwawa kwa kipigo alifanikiwa kukimbia katika chumba hicho na kwenda kujificha nje na baada ya muda mwanaume huyo alianza kutapika na pale alipoingia kutana kumsaidia ndipo alipopigwa na kuamua kukimbia kwenda kulala nje ya nyumba hiyo kwa kujiegesha katika nguzo ya umeme iliyopo nyumba ya pili karibu na nyumba ya shekhe wa mkoa Juma Alli Tagalile
Alisema kuwa asubuhi aliingia katika chumba hicho baada ya mwanaume huyo kutoka kwenda katika kilabu cha pombe za kienyeji cha Tulivu kuendelea kunywa pombe na kumkuta mtoto huyo akiwa amelala bila kutikisika .
" Mimi nilijua kama mtoto amelala tu ama amezimia ila baada ya kuwaita watu wazima akiwemo mama yangu mzazi ndipo nilipobaini kuwa mtoto wangu Ray amefariki dunia na ndipo nilipomfuata na kumweleza juu ya tukio hilo ila bado aliendelea kunywa pombe na kudai kuwa mtoto huyo amezimia kwa kelele za usiku ."
Alisema baada ya hapo mwanaume huyo alikimbia hadi Ilala kwa wakwe zake na kuomba msamaha na kusuluhishwa ugomvi wao ila wakati mtengo wa kukamatwa ukiwekwa ndipo alipokimbia kusiko julikana.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mtoto huyo akiwa amekufa katika kitanda cha wazazi wake huku chini ya chumba hicho thamani mbali mbali pamoja na vyombo vikiwa vimevunjika kutokana na ugomvi huo .
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa Pangani kata ya Makorongini Bw Salum Kibaya amethibitisha juu ya kifo cha mtoto huyo na kuwa baada ya tukio hilo ambalo lilitokea usiku wa kuamkia leo jumamosi Desemba 14 mwaka huu alilazimika kwenda kituo cha polisi cha stendi kuu ya mabasi yaendeyo mikoani na kuwajulisha juu ya tukio hilo na kufika eneo la tukio .
Bw Kibaya alithibitisha pia kuwa ugomvi kati ya wapenzi hao si wa kwanza kutokea japo kwa maelezo ya mwanamke huyo alikuwa mbioni kuolewa na mwanaume huyo na hivyo kuwa na wanaume wawili akiwemo mzazi mwenzake ambae kwa sasa anaishi eneo la Don Bosco mjini hapa.
Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa huku jeshi la polisi likiwahoji mama wa mtoto huyo ,kama wa mtuhumiwa wa mauwaji hayo ambae ni mkazi wa Mlandizi Kibaha Jijini Dar es Salaam na mama mzazi wa mtoto aliyepoteza maisha.

MBUZI AZALIWA AKIWA NA SURA YA MTU HUKO KENYA

Wakazi wa eneo la Likoni, Mombasa nchini Kenya walipatwa na mshangao mkubwa mara baada ya mbuzi mmoja kujifungua mtoto mwenye sura inayofanana na binadamu.

Tukio hilo lilifanya shughuli mbalimbali kwenye kijiji hicho kusimama huku wakazi wa eneo hilo wakiwa wanastaajabu juu ya tukio hilo la ajabu.

Friday, 13 December 2013

KENYA BINGWA WA CECAFA 2013/2014 TANZANIA YA LALIA PUA YAIBUKA MSHINDI WA 4

Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, imekamilisha furaha ya Wakenya katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa taifa hilo baada ya kuicharaza timu ya Sudan mabao 2-0 katika mchezo wa fainali za mashindano ya nchi za Afrika mashariki na Kati Cecafa.
Mechi hiyo iliyofanyika siku ya kilele cha sherehe za uhuru wa Kenya, tarehe 12 Desemba 2013, Harambee Stars walitumia vizuri sherehe hizo huku wakishangiliwa na mashabiki wao waliofurika katika uwanja wa Nyayo kuinyoa Sudan katika mchezo huo.
Nahodha wa Harambee Stars, Wanga ndiye aliyekuwa muuaji wa timu ya Sudan baada ya kufunga mabao yote mawili.
Katika mchezo wa awali ambao ulizikutanisha Tanzania na Zambia kumsaka mshindi wa tatu, Zambia iliibuka mshindi baada ya kuwalaza Kilimanjaro Stars jumla ya mabao 6-5 baada ya timu hizo kutoka sare ya goli 1-1 hadi dakika tisini za mchezo, ndipo mikwaju ya penalti ikaamuliwa kupigwa na Zambia kuibuka washindi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Harambee Stars katika kipindi cha miaka kumi na moja kutwaa kombe la Cecafa.
Mchezo wa fainali kati ya Kenya na Sudan ulichelewa kuanza kutokana na kubadilishwa muda kutoka saa 11 hadi saa 12 jioni.
Kuna taarifa kwamba kuchelewa kuanza kwa mchezo huo huenda kumesababishwa na timu ya Sudan kuzuiliwa hotelini walimokuwa wakikaa baada ya mamlaka zinazohusika kudaiwa kushindwa kulipia pango la timu hiyo.

Mjomba wa kiongozi wa Korea anyongwa

Shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA, limetangaza kuwa Jang Song-thaek, mtu mwenye nguvu kisiasa nchini humo na ambaye ni mjomba wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, amenyongwa.
Shirika hilo limesema Jang alituhumiwa kutumia vibaya madaraka, kupinga vitendo vya kiwana mapinduzi na kukengeuka kitabia.
Bwana Jang alihukumiwa na mahakama maalum ya kijeshi na kunyongwa papo hapo kama msaliti. Mapema wiki hii, picha za televisheni zilimwoonyesha Jang Song Thaek akiondolewa na walinzi wenye kuvalia sare kutoka katika mkutano wa Chama tawala cha Kikomunisti.
Wachambuzi wa mambo wanaona kunyongwa kwake kama jaribio la kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un kujiimarisha kiutawala.
Ni tukio kubwa kutokea tangu Bwana Kim amrithi baba yake, Kim Jong-Il miaka miwili iliyopita.
Shirika la habari la Korea Kaskazini, limesema Jang alikiri makosa katika mahakama ya kijeshi Alhamisi, kutaka kuiangusha serikali, na alinyongwa mara moja.
Bwana Jang, ambaye anafikirika kumjenga mpwa wake, wakati wa kipindi cha mpito wa uongozi kutoka kwa Bwana Kim Jong-il kwenda kwa mtoto wake Kim Jong-un mwaka 2011, "alikuwa mbaya kuliko mbwa" limesema shirika hilo.
Alikiri kutumia vibaya nafasi zake za uwajibikaji ili kuunda kikundi cha upinzani dhidi ya serikali na kulinda maslahi yake ya kisiasa, imesema taarifa ya shirika hilo la KCNA.
Kim Jong-un kiongozi wa Korea Kaskazini
Nchini Marekani, Ikulu ya nchi hiyo, imesema haiwezi kuthibitisha ukweli wa taarifa hizo, "lakini halina sababu za kutilia mashaka taarifa hizo"
"Kama itathibitika kuwa kweli, huu ni mfano mwingine wa ukatili uliopita kiasi, unaoendeshwa na utawala wa Korea Kaskazini. Tunafuatilia kwa karibu zaidi taarifa hizo na kushauriana na nchi washirika na marafiki katika eneo hilo.," imesema taarifa ya Ikulu ya Marekani.
Picha ya Bwana Jang akiwa mahakamani, mikono yake ikiwa imefungwa, imetolewa Ijumaa.
Kabla ya kutoweka kwa neema yake, mara kwa mara alipigwa picha akiwa pembeni mwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un
Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye amesema Korea Kaskazini imekuwa ikiendesha "utawala wa hofu"
Bwana Jang Song-thaek aliyemuoa dada wa kiongozi wa zamani wa Korea Kaskazini Kim Jong-il ambaye ni baba wa kiongozi wa sasa Kim Jong-un alijiunga na chama cha Kikomunisti mwaka 1972 na kupanda ngazi za uongozi katika chama hicho na pia akipanda ngazi ya juu kijeshi chini ya kiongozi Kim Jong-un.

3 wakamatwa kwa kupanga mechi Uingereza

Sam Sodje alikuwa mchezaji wa timu ya kitaifa ya Nigeria.
Watu watatu wanazuiliwa na polisi nchini Uingereza baada ya aliyekuwa mchezaji wa Portsmouth kumwambia mwandishi wa habari kuwa alihusika katika kupanga mechi.
Sam Sodje alirekodiwa kwenye kanda ya video na mwandishi wa habari mmoja wa jarida la Sun akizungumzia alivyompiga mchezaji wa timu hasimu usoni katika ligi ya daraja la kwanza, ili apate kadi nyekundu na kisha baadaye alipwe pauni 70,000.
Alisema pia alipangia mchezaji mwingine aweze kulipwa pauni 30,000 kwa kupokea kadi ya manjano katika mechi ya ligi.
Klabu ya Portsmouth imeelezea kushtushwa sana na madai hayo.
Katika Kanda hiyo liyorekodiwa kisiri, bwana Sodje raia wa Nigeria, pia alidai ana uwezo wa kupanga mechi za ligi kuu na kuwa yuko tayari kupanga mechi katika kombe la dunia mwaka ujao.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji wa klabu hiyo, alisema kuwa ikiwa madai haya ni ya kweli, basi ijulikane kuwa ni ya kushtua na kushangaza sana , jambo la kupanga mechi bila shaka linaathiri pakubwa maadili ya mchezo wa soka.
Sodje hachezei tena klabu ya Portsmouth lakini itambidi ashirikiane na maafisa wakuu kwa uchunguzi.
Sodje aliondolewa uwanjani katika dakika ya 50 wakati wa mchuano kati ya Portsmouth na Oldham Athletic kwenye ligi ya daraja la kwanza tarehe 23 Februari mwaka 2013.

Katumbi na matarajio ya TP Mazembe

Mmiliki na mwenyekiti wa timu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo Moise Katumbi amesema ana mpango wa kuiimairisha timu hiyo ili iwe na nguvu ya kushiriki katika mashindano ya kidunia, Katumbi anaamini kuwa anaweza kuifikisha timu hiyo katika ngazi ya fainali za kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu.
Pamoja na TP Mazembe kushindwa katika michuano ya kombe la shirikisho la CAF lakini bado Katumbi anasema anajiandaa vyema na msimu ujao na mashindano mengine."Malengo yetu ni kuleta ushindani mkubwa na ninaamini tunaweza kufikia mafanikio kwa kile tulichonacho sasa"alisema Katumbi.
Katumbi pia ameiambia BBC kuwa iwapo wataimarisha zaidi timu yao na kwamba haoni ni kwanini siku moja TP Mazembe siku moja wasishinde kombe la dunia.
Mwaka 2010, timu hiyo ya soka ya Mazembe ndio iliyokuwa klabu ya kwanza toka bara la Afrika kutinga fainali katika mashindano ya kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu lakini wakaondolewa na klabu ya Inter Millan ya Italia.
Baada ya michuano hiyo ya michuano hiyo ya shirikisho timu hiyo toka mji wa Lubumbashi nchini Demokrasia ya Congo wanatarajiwa kurejea tena katika michuano ya ligi ya mabingwa mwaka ujao.
Tambo hizi za Mazembe ni kutokana na vipaji vya kutosha kutoka katika shule ya vipaji vya michezo ambapo wanatarajia baada ya miaka mitatu wantakuwa na wachezaji wenye uwezo wa kuwafikisha na kushinda kombe la dunia.
Hata hivyo Katumbi kiongozi wa miongoni mwa timu tajiri barani Afrika amesema kuwa ameweza kuhakikisha fedha zinapatikana ili kuimarisha kikosi chake,kutengezeza uwanja mpya na wa kisasa ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege ya timu.
Mipango yake katika kupata wachezaji wa kimataifa inaendelea ambapo kwa sasa anawachezaji nchi za nje ambapo kwa ana wachezaji kutoka nchi za Tanzania, Ghana, Zambia, Cameroon, Botswana na hivi karibuni amesajili kutoka Malawi.
Timu hii ya TP Mazembe ni miongoni mwa timu ambazo wachezaji wake wanalipwa vizuri kwa viwango vya Afrika ikiwa ni jitihada za Katumbi kupunguza kaksi ya vipaji vya Afrika kupotelea ulaya.
"Wachezaji wazuri wa Afrika wanakwenda ulaya kwa sababu ya malipo mazuri kutokana na kutolipwa vizuri hapa Afrika" anasema Katumbi.
Katumbi anasema kuwa sera yao ni kuwachukua wachezaji toka nchi za Afrika ili kuonyesha umoja ndania ya bara hilo na kwamba Afrika ni nnzuri lakini kinachotakiwa ni umoja hasa kutokana na mapigano ambayo yamekuwa yakitokea kila siku katika bara la Afrika.

Kenya yasherehekea miaka 50 ya Uhuru

Kenya inasherehekea miaka 50 ya uhuru walioupata chini ya utawala wa Uingereza.
Mamia ya raia na wageni mbali mbali wamehudhuria katika sherehe hizo zilizofanyika katika mji mkuu wa Nairobi.
Wageni mbali mbali pamoja marais wa mataifa mbali mbali wamehudhuria sherehe hizo akiwemo rais Nigeria Godluck Jonathan wa Nigeria, Jakaya Kikwete wa Tanzania, Joseph Kabila wa DRC, Pierre Nkurunziza wa Burundi, Ali Bongo wa Gabon, Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka.
Usiku wa kuamkia Alhamis bendera ya Kenya ilipandishwa katika eneo hilo hilo siku bendera ya uhuru ilipopandishwa wakati nchi hiyo inapata uhuru katika bustani ya Uhuru Desemba 12, 1963.
Siku hiyo ya uhuru Rais Jomo Kenyatta, baba yake rais wa sasa Uhuru Kenyatta alitawazwa kuwa kiongozi wa nchi hiyo.
KUNA dalili za wazi huenda Baraza la Mawaziri la Rais Jakaya Kikwete kufanyiwa mabadiliko hasa baada ya malalamiko kutoka kwa viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye na Abdulrahama Kinana, ambao wamefikia hatua ya kutaka baadhi ya mawaziri kuitwa kujieleza katika Kamati Kuu ya Chama chao kuhusu utendaji wao wa kazi.
Kati ya mambo yanayoashiria kuwapo kwa uwezekano wa baraza la mawaziri kufanyiwa mabadiliko ni hatua ya mapema wiki hii, ya Rais Kikwete kumteua Dk. Asha Rose Migiro kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Uteuzi huo ulitangazwa Jumanne wiki hii na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Florens Turuka, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyoeleza kwamba uteuzi huo umeanza rasmi juzi Jumatatu.
Kwa kawaida, wengi wa wabunge ambao Rais Kikwete amekuwa akiwateua kuwa wabunge wameishia kuwa mawaziri na uteuzi huu wa Migiro umeleta hisia hizo.
Tangu achaguliwe kuwa Rais katika awamu yake ya pili ya uongozi, ukiondoa uteuzi huu wa Migiro, Kikwete tayari ameteua wabunge sita na kati yao,  wanne ni mawaziri katika serikali yake.
Wabunge ambao Kikwete amewateua kuwa mawaziri tayari ni Profesa Sospeter Muhongo, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Janet Mbene na Shamsi Vuai Nahodha.
Wabunge ambao Kikwete aliwateua lakini hawakupata uwaziri ni Zakhia Meghji na James Mbatia kutoka chama cha NCCR-Mageuzi.
Kwa sasa, Dk. Migiro, msomi wa kiwango cha shahada ya uzamivu katika sheria na Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN), ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya  Taifa katika  dara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM.
Uteuzi huu wa Migiro umekuja pia katika kipindi ambacho Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ameibua hoja ya kutaka serikali ichukue hatua dhidi ya mawaziri wanaotajwa kutokuwa wachapakazi.
Kinana ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM na inaelezwa kuwa ni sawa na ‘sikio’ la Kikwete kwa vile amekuwa meneja wake wa kampeni katika vipindi vyote viwili alivyowania urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na 2010.
Kutokana na ushawishi huo wa Kinana, inaelezwa kuwa anaweza kusukuma kufanyiwa mabadiliko kwa baraza la mawaziri ili kazi ya siasa kama kiongozi mtendaji mkuu wa CCM iende vema, hasa katika mwelekeo wa maandalizi ya siasa za mwaka 2015, wakati wa UChaguzi Mkuu ujao.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/baraza-la-mawaziri-kuvunjwa#sthash.QY2HcXVN.dpuf

- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/baraza-la-mawaziri-kuvunjwa#sthash.QY2HcXVN.d

- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/baraza-la-mawaziri-kuvunjwa#sthash.QY2HcXVN.dpufhdiaf i