Friday 13 December 2013

KENYA BINGWA WA CECAFA 2013/2014 TANZANIA YA LALIA PUA YAIBUKA MSHINDI WA 4

Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, imekamilisha furaha ya Wakenya katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa taifa hilo baada ya kuicharaza timu ya Sudan mabao 2-0 katika mchezo wa fainali za mashindano ya nchi za Afrika mashariki na Kati Cecafa.
Mechi hiyo iliyofanyika siku ya kilele cha sherehe za uhuru wa Kenya, tarehe 12 Desemba 2013, Harambee Stars walitumia vizuri sherehe hizo huku wakishangiliwa na mashabiki wao waliofurika katika uwanja wa Nyayo kuinyoa Sudan katika mchezo huo.
Nahodha wa Harambee Stars, Wanga ndiye aliyekuwa muuaji wa timu ya Sudan baada ya kufunga mabao yote mawili.
Katika mchezo wa awali ambao ulizikutanisha Tanzania na Zambia kumsaka mshindi wa tatu, Zambia iliibuka mshindi baada ya kuwalaza Kilimanjaro Stars jumla ya mabao 6-5 baada ya timu hizo kutoka sare ya goli 1-1 hadi dakika tisini za mchezo, ndipo mikwaju ya penalti ikaamuliwa kupigwa na Zambia kuibuka washindi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Harambee Stars katika kipindi cha miaka kumi na moja kutwaa kombe la Cecafa.
Mchezo wa fainali kati ya Kenya na Sudan ulichelewa kuanza kutokana na kubadilishwa muda kutoka saa 11 hadi saa 12 jioni.
Kuna taarifa kwamba kuchelewa kuanza kwa mchezo huo huenda kumesababishwa na timu ya Sudan kuzuiliwa hotelini walimokuwa wakikaa baada ya mamlaka zinazohusika kudaiwa kushindwa kulipia pango la timu hiyo.

No comments: