Thursday 19 December 2013

WABUNGE WAUMBUANA HADHARANI

Dodoma. Wabunge jana waliumbuana kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma huku Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe akituhumiwa kuagiza kubadilishwa kwa tiketi ya ndege ya Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Joyce Mukya ili afupishe ziara yake ya kikazi huko Marekani na kwenda Uarabuni kwa shughuli binafsi.(EL).Mbali ya Mbowe, Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM) anadaiwa kuchukua posho ya Kamati ya Hesabu za Bunge (PAC), kwa safari ya kwenda Dubai na wenzake lakini badala yake akaenda Mbeya kwenye ziara za chama chake.Malumbano hayo yaliibuka jana baada ya Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), kuomba mwongozo wa Spika akitaka kufahamu kauli ya ofisi yake kwa Mbowe kutumia nafasi yake kumrudisha mbunge ambaye ameshatumia fedha za Serikali.Alidai kwamba Mbowe aliagiza Mukya aanze safari Desemba Mosi, mwaka huu kutoka New York, Marekani ili aende Dubai, Falme za Kiarabu (UAE) kabla ya kwenda Dar es Salaam, Desemba 3, mwaka huu.Alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo j

http://ukomboz.blogspot.com/2013/12/wabunge-waumbuana-hadharani_1390.html

No comments: