Monday, 9 December 2013

Kocha wa Azam aenda likizo


Dar es Salaam.
Kocha mpya wa Azam, FC Joseph Omog ameondoka nchini mwishoni wa wiki kuelekea Cameroon na kumwachia majukumu msaidizi wake Kali Ongala.
Akizungumza jijini Dar es Salaa, Msemaji wa Azam FC, Jafar Iddi alisema Omog atarejea tena nchini Desemba 20 ili kuendelea na kazi ya kukiandaa kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mzunguko ujao wa ligi na mashindano ya kimataifa.
“Kocha wetu mkuu amesafiri kwenda nchini kwake Cameroon kwa ajili ya kumalizia likizo yake ambako atakaa kwa muda wa wiki mbili na atarejea nchini tarehe 20 Desemba kuendelea na majukumu yake,”alisema Iddi.
Alisema,”Kabla ya kuondoka, kocha ameacha programu ya wiki mbili kwa wasaidizi wake Kally Ongala na Ibrahim Shikanda ambao watakuwa wakisaidiwa pia na kocha wa timu yetu ya vijana Vivek Nagul.”
Kabla ya kutua Azam, Kocha Omog alikuwa kocha wa AC Leopards ya DR Congo, ambapo aliiwezesha kutwaa vikombe vya Chama cha Soka cha DR Congo na Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Azam itaiwakilisha Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

No comments: