Dodoma. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
za Mitaa (Laac), imeilipua Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi) kwa madai ya kuwa sehemu ya Mtandao wa Ufisadi
serikalini.
Tamisemi inaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia anayesaidiana na manaibu waziri
wawili, Aggrey Mwanry na Majaliwa Kassim Majaliwa.
Halikadhalika kamati hiyo ya Bunge imesema, zipo
dalili za wazi za kuwapo kwa mtandao wa kutisha wa kifisadi
unawashirikisha baadhi ya watendaji wa halmashauri nchini, hazina na
Tamisemi.
Tuhuma hizo zilitolewa Bungeni jana na Mwenyekiti
wa Laac,Rajab Mbarouk wakati akiwasilisha taarifa ya hoja za kamati
kuhusu hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,2012.
Alisema bado kuna ubadhirifu,ufisadi na utovu wa
nidhamu wa hali ya juu wa matumizi ya fedha za umma kutokana na Tamisemi
kutosimamia ama yenyewe kuhusika moja kwa moja na ufisadi huo.
“Mfano mwaka 2011/12, Sh1.6 bilioni zilitumika nje
ya bajeti iliyoidhinishwa katika halmashauri 38 na Sh2.6 bilioni
zilihamishwa kutoka akaunti moja kwenda nyingine bila
kurudishwa,”alisema.
Kamati hiyo imebaini kwamba upo mtindo wa Serikali
kutuma kwa halmashauri kiasi kikubwa cha fedha kuliko kiasi cha fedha
kilichoidhinishwa na Bunge katika fungu husika wakati wa upitishaji
bajeti.
Kamati hiyo imetolea mfano wa Sh2 bilioni
zilizotumwa Halmashauri ya Jiji la Tanga na Sh500 milioni zilizotumwa
katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe ikiwa ni zaidi ya kiasi
kilichoidhinishwa na Bunge.
“Kitendo hiki ambacho kinafanyika kwa ushirikiano
wa hali ya juu wa Hazina,Tamisemi na Halmashauri kinaashiria kuwapo
mtandao wa kutisha wa kifisadi baina ya mamlaka hizo,”alisema.
Kamati hiyo imeituhumu pia Tamisemi inayoongozwa
na Waziri Hawa Ghasia, kuwahamisha haraka watumishi wanaotuhumiwa
kufanya ubadhirifu kutoka hamashauri moja kwenda nyingine.
“Kamati imebaini kwamba Tamisemi imekuwa ikitumia
mtindo huu kuwalinda watumishi mafisadi ndani ya halmashauri na kuifanya
kamati iamini Tamisemi ni sehemu ya mtandao huu,”imesema.
Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kwa
makusudi,Tamisemi imekuwa ikieneza saratani hiyo ya ufisadi kwenye
halmashauri nyingi iwezekanavyo na kuitaka Serikali kuachana na mtindo
huo.

No comments:
Post a Comment