Kamanda huyo, Generali Carlos Alberto dos Santos
Cruz, anasema kwamba wanajeshi wake wanajiandaa kupambana na waasi wa
FDLR walio Katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Kamanda wa wanajeshi wa Umoja wa mataifa katika
Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, anasema kuwa wanajeshi wake wameanza
kupambana na waasi wa Kihutu kutoka Rwanda pamoja na makundi mengine ya
waasi Mashariki mwa nchi.
Kundi hilo, lilianzishwa na wapiganaji wa kihutu
waliokimbilia Congo Mashariki kutoka Rwanda wakati wa mauaji ya kimbare
mwaka 1994.Mwezi jana wanajeshi wa UN kwa kutumia nguvu waliweza kuwashinda waasi wa M23 waliokuwawanaendesha harakati zao Mashariki mwa Congo.
No comments:
Post a Comment