KOSA la kumzuia straika Amisi Tambwe
lililofanywa na mabeki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin
Yondani hadi akapiga pasi kwa mfungaji Betram Mombeki, sasa linafanyiwa
kazi na kikosi cha Simba.
Mombeki alifunga bao hilo dakika ya 54 baada ya
kupokea pasi murua ya Tambwe ambaye aliwazidi ujanja Yondani na
Cannavaro ambao walijipanga vibaya kwa kumzuia Tambwe lakini straika
huyo aliwazidi ujanja na kumpa pasi mfungaji.
Katika pambano hilo la Ligi Kuu Bara lililochezwa Oktoba 20, mwaka huu kaika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0 hadi mapumziko lakini Simba ilisawazisha mabao yote kipindi cha pili.
Katika pambano hilo la Ligi Kuu Bara lililochezwa Oktoba 20, mwaka huu kaika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0 hadi mapumziko lakini Simba ilisawazisha mabao yote kipindi cha pili.
Kwa muda mrefu kwenye mazoezi ya Simba mwishoni
mwa wiki iliyopita, Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic ameonekana
akiwahimiza mabeki wake hasa wa kati kusimama katika nafasi sahihi
wakati timu inaposhambuliwa.
Logarusic alionekana akitilia mkazo sehamu ya
kusimama mabeki wake na mara kwa mara alikuwa akiwaelekeza kwa ukali
baadhi ya mabeki waliokuwa wakirudia makosa ya kutokuwapo sehemu husika.
Kocha huyo alienda mbali zaidi kwa kuwafundisha mabeki wake namna ya
kusimama wanapokuwa wanakaba jambo lililokuwa likishangiliwa na
mashabiki wachache wa Simba waliohudhuria mazoezi hayo.
Muda mfupi baada ya mazoezi hayo, Logarusic raia
wa Croatia aliliambia Mwanaspoti; “Beki yeyote mzuri lazima awe anajua
mahala sahihi pa kusimama na usimamaji wake unapaswa kuwa madhubuti
ndiyo maana umeona nawasisitizia.”
No comments:
Post a Comment