Mimi ni miongoni mwa mamilioni ya
watu ambao walivutiwa na maisha ya Nelson Mandela. Tukio langu la kwanza
la kisiasa nililolifanya ambalo lilihusu sera au siasa lilikuwa ni
mgomo dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Nia yake njema ya kukabidhi madaraka na kutoa
msamaha kwa wote waliomfunga inatupa mfano ambao kila mmoja anapaswa
kujifunza katika ngazi ya kitaifa na hata kwenye maisha binafsi. Kwa
sababu alifanya kila kitu kwa furaha na ucheshi, na akiwa na uwezo wa
kujikosoa mwenyewe, hivyo zinamfanya aonekane kuwa mtu wa tofauti.
Aliwahi kusema: “Mimi siyo mtakatifu, labda kama unamfikiria mtakatifu
mtenda dhambi ambaye anaendelea kujaribu.”
Mimi ni miongoni mwa mamilioni ya watu ambao
walivutiwa na maisha ya Nelson Mandela. Tukio langu la kwanza la kisiasa
nililolifanya ambalo lilihusu sera au siasa lilikuwa ni mgomo dhidi ya
ubaguzi wa rangi. Nilijifunza maneno na maandishi yake.
Siku ile ambayo aliachiwa kutoka gerezani ilinipa
wazo namna ambavyo watu wanaweza kufanya wanapokuwa wanalindwa na
tumaini na siyo hofu. Na kama ilivyo kwa watu wengi duniani kote, siwezi
kufikiri kwa mapana maisha yangu yatakuwaje bila mfano ambao Nelson
Mandela ameuweka. Kwa kuwa bado ningali hai, nitafanya kila
linalowezekana kujifunza kutoka kwake.
Kwa Graca Machel na familia yake, Michelle na mimi
mwenyewe tunatoa salamu zetu za maombolezo kwa namna
walivyotushirikisha kuhusu Mandela. Ninatumaini kuwa muda walioutumia na
Mandela wiki za mwisho zilileta amani na faraja kwa familia yake.
Kwa watu wa Afrika Kusini, tunajifunza kutoka kwa
mfano wa kuheshimiwa, kupenda mapatano na uhuru wa kufikiri ambao
mmeufanya. Afrika Kusini iliyo na amani, huo ni mfano kwa dunia, na
ndiyo urithi wa Madiba kwa taifa alilolipenda.
Kuna uwezekano kwamba hatuwezi kuona tena mambo
ambayo Nelson Mandela aliyapenda. Kwa hiyo ni wajibu wetu kuendeleza
mfano ambao aliuweka. Kufanya uamuzi usiotokana na chuki, bali upendo;
kwa kutambua tofauti ambayo mtu mmoja anaweza kuileta, kuupigania wakati
ujao ambao una thamani sawa na sadaka aliyoitoa.
Kwa sasa, kupumzike kidogo na kushukuru kutokana
na ukweli kwamba Nelson Mandela aliishi, mtu ambaye aliichukua historia
mikononi mwake na kupindisha mazoea ya dunia kuhusu haki. Mungu aibariki
historia yake na kumuweka katika amani.
No comments:
Post a Comment