Rais Omar al-Bashir amehudhuria sherehe za kuapishwa kwa makamu wa
marais wawili walioteuliwa hivi karibuni pamoja na wasaidizi na mawaziri
wapya, ambao wote wanatoka Chama tawala cha National Congress CNP.
Mabadiliko ya baraza la mawaziri nchini Sudan yamekuja baada ya nchi
hiyo kuendelea kukumbwa na hali ya kukosekana kwa utulivu wa kisiasa.
Makundi ya waasi wa Sudan ambao mara kwa mara wanalalamikia hali ya
kuwekwa kando na maendeleo yasiyo na uwiano katika maeneo nje ya
Khartoum, wanaendelea na mapambano, huku hali ya kuzorota kwa uchumi
mjini Khartoum na kupanda kwa bei za bidhaa zikisababisha malalamiko na
vifo vya watu wengi katika mwezi Septemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment