eshi la Sudan Kusini limesema haliudhibiti tena mji muhimu wa Bor, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa jeshi hilo kukiri kushindwa katika mapigano yanayoendelea kwa siku ya nne sasa kati ya makundi pinzani ya wanajeshi. Kifaru cha kijeshi kikifanya doria mjini Juba Mapigano hayo makali yanatishia kuitumbukiza nchi hiyo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Msemaji wa Jeshi la Sudan Kusini, Kanali Philip Aguer, amesema leo (19.12.2013) kuwa wanajeshi waasi wanaomtii aliyekuwa makamu wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar wameutwaa mji wa Bor.Amesema viongozi katika mji huo ambao ni mji mkuu wa jimbo la Jonglei, hawapokei simu zao, hatua inayoifanya serikali kuu kuamini kwamba wamejiunga na waasi.Kanali Aguer amesema wamepoteza udhibiti wa mji wa Bor na kwamba milio ya risasi imesikika usiku kucha ingawa bado hawana taarifa kuhusu waathirika au watu walioyakimbia makaazi yao kwa sababu operesheni za kijeshi bado zinaendelea.Watu 19 wauawa BorMsemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Martin Nesi
http://ukomboz.blogspot.com/2013/12/mji-wa-bor-sudan-kusini-wadhibitiwa-na.html
No comments:
Post a Comment