Kavishe aliongeza kuwa mechi hii ni
maalum kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo imeendeshwa
kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu
zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Kilimanjaro Premium Lager
ilitenga kiasi cha shilingi milioni 100 zinazoshindaniwa na Simba
na Yanga kupitia mashabiki wake na tarehe 21 Desemba ndio utakuwa mwisho wa
kampeni ya Nani Mtani Jembe ambapo baada ya mechi fedha hizo zitagawanywa
kwa kila timu kulingana na matokeo ya kura za mashabiki na klabu zitajiamulia namna
ya kutumia fedha hizo.
Kampeni hii imeleta msisimko mkubwa
sana kati ya mashabiki na hadi sasa matokeo ya kampeni hii yanaonyesha kwamba
Yanga wanaongoza wakiwa na kiasi cha shilingi milioni 76 huku Simba wakiwa na
kiasi cha shilingi milioni 24
Mashabiki wa Simba na Yanga
wanaoshiriki katika kampeni ya Nani Mtani Jembe wanaendelea kunufaika zaidi na
zawadi kabambe zilizoandaliwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ili kuongeza
msisimko na ushiriki katika kampeni hiyo ambapo mashabiki watatu wa Simba na
mashabiki watatu wa Yanga wanajishindia kiasi cha shilingi 300,000/= kila mmoja
katika droo zinazofanyika mara moja kila wiki. Droo kubwa itafanyika tarehe 21
Desemba. Ambapo katika droo hiyo kubwa shilingi milioni 6 zitatolewa kama
zawadi kwa washindi wawili - mmoja shabiki wa Yanga na mwingine shabiki
wa Simba ambapo kila mmoja atajishindia shilingi milioni tatu.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro, Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro George Kavishe, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala na
Mkurugezi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba wakioshela alama ya dole
baada ya kutangaza Simba na Yanga kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe
itakayochezwa Desemba 21 jijini Dar es salaam (Executive Solutions)
No comments:
Post a Comment