Monday, 9 December 2013

Wajasiriamali Tanzania kushiriki maonesho ya Juakali

juakali
WAJASIRIAMALI 250 wameondoka jana kuelekea nchini Kenya kushiriki maonesho ya Juakali na Nguvukazi yanayoshirikisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mjumbe wa mandalizi kutoka Wizara ya Kazi na Ajira, Bonavetura Mwalongo, alisema maonesho hayo ya siku saba yataaza kesho.
Alisema safari ya wajasiriamali hao imeratibiwa na wizara nne ambazo ni Biashara na Viwanda; Uchukuzi; Afrika Mashariki na wenyeji wizara ya Kazi na Ajira.
Mwalongo alisema lengo la serikali ni kuikuza sekta binafsi ndani ya EAC na kufafanua zaidi kwamba miongoni mwa wajasiriamali waliosafiri wamo waganga wa tiba asili.
Naye bingwa wa kutibu kisukari kwa njia asili, Dk. Juma Juma, alisema atatoa ushuhuda unaoonyesha kuwa ugonjwa huo unaweza kupona haraka kwa tiba asili.
Ofisa Mkuu wa Huduma na Elimu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Julius Mjenga, alisema wamewapatia elimu ya kulipa kodi, ili iwasaidie watakapokutana na maofisa wanaosimamia sheria za mapato.

No comments: