Majeshi ya Ufaransa katika
Jamhuri ya Afrika ya Kati, yanaongeza kasi ya juhudi zao dhidi ya vurugu
na kuzieneza katika sehemu nyengine za taifa hilo ili kurejesha utulivu
baada ya mapigano ya kidini.
Wanajeshi zaidi wa Ufaransa walishika doria katika mji mkuu Bangui huku wengine wakiingia nchini humo kupitia Cameroon.Ufaransa, inaongeza idadi ya wanajeshi wake nchini humo hadi 1,600, kuisaidia wanajeshi wanaolinda Amani kukabiliana na vurugu kati ya waisilamu na wakristo.
Afrika ya Kati imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu Michel Djotodia kumng’oa mamlakani aliyekuwa Rais Francois Bozize.
Djotodia amejitangaza kuwa kiongozi wa kwanza wa waisilamu katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya wakristo.
Kundi la waasi la Seleka ambalo lilimuingiza mamlakani Djotodia, linatuhumiwa kwa kuwaua wakristo .
Duru zinasema kuwa mamia ya watu waliuawa wiki jana katika vita vinavyochochewa na waasi wa Seleka.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amesema viongozi wa Afrika lazima wahakikishe kuwa wanadhibiti ulinzi na usalama katika mataifa yao.
No comments:
Post a Comment